WANAWAKE WAJASIRIAMALI WAKUMBUSHWA KUJISAJILI BRELA KUEPUKA KUTAPELIWA

Wanawake Wajasiriamali katika biashara mbalimbali waliojitokeza katika hafla ya iliyofanyika Sea cliff Masaki Jijini Dar es Salaam  ya kuwatambua Wanawake Wajasiriamali walionufaika na Taasisi ya Wanawake Wajasiriamali (WCW).

****************

SERIKALI imesema itaendelea kuwainua wanawake kwenye sekta mbalimbali ili waweze kujikwamua kiuchumi nakuharakisha Maendeleo hasa katika harakati za kuhakikisha mwanamke anajikomboa kiuchumi.

Hayo ameyasema leo Jijini Dar es Salaam na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa alipokuwa akimuwakilisha Waziri waViwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji katika mkutano wa taasisi isiyokuwa yakiserikali yenye lengo la kuwainua wanawake nchini Womeni Creating Wealth(WCW).

Aidha Bw. Nyaisa amewataka kuwa wanawake nchini wenye nia ya kuinua biashara na kujiepusha matapeli ni wakati sahihi kujisajili na BRELA .

"Kumwezesha mwanamke ni kuisaidia jamii ili kuweza kukuza uchumi, Brela ni taasisi ya kukuza biashara,na tunawataka wanawake wote kusajili biashara zao hapa,na kujiepuka na kutapeliwa". Ameongeza

Pamoja na hayo Bw. Nyaisa ametumia mkutano huo kuwataka wanawake hao kuhakikisha wanakuwa na banda lao la kuonesha kazi zao za ujasiliamali kupitia maonesho mbalimbali ili kuwainua wanawake wengine.

Kwa upande wake Meneja wa WCW Bi. Anabahati Mlay amesema taasisi hiyo imefanikiwa kuwainua wanawake mbalimbali na kuwajengea kiuchumi

"Tumewajengea wanawake mbalimbali kiuchumi toka 2016 wanawake wamekuwa wakinufaika". Amesema

Naye Bw. Mosi Hassani ambaye ni mjasiamali ameishukuru WCW kwa hatua yake ya kuwainua wanawake nchini.

"Nimepata fursa kwenye masoko ,nawashukuru sana "

Meneja mkuu wa nchini Tanzania wa Taasisi ya Wanawake Wajasiriamali (WCW) Anabahati Mlay akiongea machache juu ya malengo ya taasisi hiyo imefanikiwa kuwainua Wanawake na Kuwajengea kiuchumi
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa Leo Novemba 16,2023 akizungumza na Wanawake Wajasiriamali (WCW) pamoja na Wanahabari ukumbi wa Seacliff Masaki  Jijini Dar es Salaam na kuwakumbusha Wajasiriamali hao kuhakikisha biashara zao zinatambulika kwa njia ya kujisajili Brela pamoja na kufanya biashara zenye tija na faida kubwa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم