SERIKALI YAZINDUA MRADI WA VICHANJA VYA KUANIKIA SAMAKI BAGAMOYO

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Bw. Prudence Constantine akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Vichanja 10 vya kuanikia Samaki kwa kikundi cha "Simama Wanawake na Maendeleo"-(SIWANA) katika halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani ambayo yatawasaidia kukaushia samaki kwa njia ya kisasa. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023.

******************

NA EMMANUEL MBATILO, BAGAMOYO

SERIKALI ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Ubalozi wa Japan pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa (UNDP), wamezindua Mradi wa Vichanja 10 vya kuanikia Samaki kwa kikundi cha "Simama Wanawake na Maendeleo"-(SIWANA) katika halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani ambayo yatawasaidia kukaushia samaki kwa njia ya kisasa.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika leo Novemba 17,2023, Bagamoyo, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Bw. Prudence Constantine ambaye alimwakilisha Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Mhe.Jenista Mhagama amesema kuwa katika kuhakikisha utekelezaji wa azma ya Serikali katika kuwainua Wananchi wake kiuchumi, imekua ikiandaa mipango mbalimbali kwa kushirikiana na wahisani wa maendeleo ili kuweka miundombinu itayowezesha Kufanya Shughuli zenu kwa wepesi na ufanisi zaidi.

Amesema moja kati ya Mipango hiyo ya Serikali ni kuandaa Mradi huu wa Kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu Nchini.

" Takriban Kazi zote zilizopangwa kutekelezwa katika Mradi huu zimekamilika kama ilivyoelewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu ikiwa ni pamoja na hii ambayo leo hii imetukutanisha". Amesema Bw. Constantine

Aidha amewataka wataalam ambao wamepata mafunzo mbalimbali ya kukabiliana na wahalifu baharini wawe tayari kwa ajili ya kuitika wito ili kutumia ujuzi huo kwa maslahi mapana ya nchi.

"Serikali ipo tayari katika kuhakikisha kikosi kasi hicho kinapatiwa vifaa vinavyohitajika ili kutimiza wajibu wake. Taasisi ambazo zimetoa wataalamu hao wawe tayari kuwaruhusu wakati kikosi kazi hicho kitapoitwa kwa ajili ya kazi watayopangiwa". Ameeleza

Pamoja na hayo amewataka wale waliopatiwa mafunzo kupitia vyama vya ushirika na vikundi vya maendeleo kuyazingatia mafunzo hayo ili kuleta mabadiliko chanya katika vikundi vyao, ili kukuza kipato cha vyama na mtu binafsi.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Mipango- Tawi la Mwanza, Prof. Juvenile Nkonoki amesema kuwa wanakabidhi vichanja hivyo kutokana na kikundi cha SIWANA kuwa imara na juhudi ambazo wanazionesha katika kuhakikisha wanajikomboa kiuchumi.

"Uimara huu tuliutambua wakati wa ukusanyaji wa takwimu za uandishi na upembuzi yakinifu wa kiwanda kuchakata Dagaa na wakati wa mafunzo kwa vikundi vya wavuvi na ushirika hapa Bagamoyo". Amesema Prof. Nkonoki

Pamoja na hayo amewapongeza wadau wote ambao wameweza kujitokeza na kufanikisha zoezi hilo kwa manufaa makubwa ya wananchi wa Bagamoyo pamoja na wa maeneo mengine yaliyopo karibu.

Nae Muweka Hazina wa Kikundi cha SIWANA, Bi. Fadhira Mtelekezo ameishukuru Serikali kwa kuwaletea mradi huo kwani utaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha kuanika dagaa kwa urahisi na kwa njia salama.

Hata hivyo kikundi hicho kimeiomba Serikali kupitia Halmashauri ya Bagamoyo kuweza kuwafikishia karo ambalo litawasaidia kutupia majitaka pindi wanapofanya usafi katika vichanja hivyo.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Bw. Prudence Constantineakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Vichanja 10 vya kuanikia Samaki kwa kikundi cha "Simama Wanawake na Maendeleo"-(SIWANA) katika halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani ambayo yatawasaidia kukaushia samaki kwa njia ya kisasa. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Bw. Prudence Constantine akikagua Vichanja 10 vya kuanikia Samaki kwa kikundi cha "Simama Wanawake na Maendeleo"-(SIWANA) mara baada ya kuzindua mradi huo Novemba 17,2023 Bagamoyo mkoani Pwani.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Bw. Prudence Constantine akikagua Vichanja 10 vya kuanikia Samaki kwa kikundi cha "Simama Wanawake na Maendeleo"-(SIWANA) mara baada ya kuzindua mradi huo Novemba 17,2023 Bagamoyo mkoani Pwani.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Bw. Prudence Constantine akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Vichanja 10 vya kuanikia Samaki kwa kikundi cha "Simama Wanawake na Maendeleo"-(SIWANA) katika halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani ambayo yatawasaidia kukaushia samaki kwa njia ya kisasa. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023
Mkuu wa Chuo cha Mipango- Tawi la Mwanza, Prof. Juvenile Nkonoki akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Vichanja 10 vya kuanikia Samaki kwa kikundi cha "Simama Wanawake na Maendeleo"-(SIWANA) katika halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani ambayo yatawasaidia kukaushia samaki kwa njia ya kisasa. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023
Mwakilishi wa Ubalozi wa Japan Bi. Chie Miyashita akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Vichanja 10 vya kuanikia Samaki kwa kikundi cha "Simama Wanawake na Maendeleo"-(SIWANA) katika halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani ambayo yatawasaidia kukaushia samaki kwa njia ya kisasa. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023
Mwakilishi wa UNDP, Bw. Emmanuel Nnko akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Vichanja 10 vya kuanikia Samaki kwa kikundi cha "Simama Wanawake na Maendeleo"-(SIWANA) katika halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani ambayo yatawasaidia kukaushia samaki kwa njia ya kisasa. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023
Diwani wa Kata Dunda-Bagamoyo Bw. Amiry mpwimbwi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Vichanja 10 vya kuanikia Samaki kwa kikundi cha "Simama Wanawake na Maendeleo"-(SIWANA) katika halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani ambayo yatawasaidia kukaushia samaki kwa njia ya kisasa. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023
Muweka Hazina wa Kikundi cha SIWANA, Bi. Fadhira Mtelekezo akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Vichanja 10 vya kuanikia Samaki kwa kikundi cha "Simama Wanawake na Maendeleo"-(SIWANA) katika halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani ambayo yatawasaidia kukaushia samaki kwa njia ya kisasa. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم