Tanzia : MFANYABIASHARA MAARUFU MUSOMA FOOD AFARIKI DUNIA

Mfanyabiashara wa nafaka mkoa wa Shinyanga Boniphace Said Kate Makilagi maarufu Musoma Food amefariki dunia. 

Taarifa zinasema Musoma Food amefariki dunia jijini Mwanza leo Jumatatu Aprili 3,2023 akiwa Hotelini. 

Kwa mujibu wa taarifa ya familia tarehe 27.5.2021 Said Makilagi alipata ajali ya gari huko Mpanda Rukwa akapelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya matibabu na kutokana na afya yake kutetereka alikuwa akipatiwa matibabu Bugando, Kenya na India. 


Hata hivyo  kutokana na matibabu  hayo alipata nafuu na kwa nyakati tofauti alikuwa anapata maumivu ya kichwa na mnamo tarehe 3.4.2023 akiwa jijini Mwanza aliugua ghafla jijini akafariki dunia.
R.I.P Musoma Food

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم