MAMA MZAZI WA ERICK KABENDERA AFARIKI DUNIA

Mama mzazi wa Mwandishi Erick Kabendera, Verdiana Mjwahuzi amefariki Dunia leo Jumanne Desemba 31, 2019 katika Hospitali ya Amana Da es Salaam  alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.



Bi. Verdiana alionekana hadharani mara ya mwisho  Disemba 13 Mwaka huu akiomba mwanae aachiwe huru kwakuwa anamtegemea kwa matibabu.

Erick ambaye kwa sasa yuko rumande katika gereza la Segerea, Dar es Salaam, alikamatwa Julai 2019 kwa makosa ya utakatishaji fedha, kukwepa kodi na kushiriki katika genge la uhalifu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم