PAPA FRANCIS AHOFIA MAKASISI WA JINSIA MOJA

Papa Francis amesema mapenzi ya jinsia moja kwa makasisi ni "jambo kubwa" na ambalo linampa "hofu".


Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani ametoa kauli hiyo katika mahojiano na Mmishenari kutoka Uhispania kuhusu wito wa kidini. Mahojiano hayo ni sehemu ya kitabu kinachoandikwa na mmishenari huyo.

Papa amesema mahusiano ya jinsia moja ni jambo la "fasheni", na ametaka makasisi kutii viapo vyao vya utawa (kutojihusisha na mapenzi).


Papa Francis amesema kanisa katoliki linapaswa kuwa "imara" wakati wa kuchagua watu watakaokua makasisi.

"Hili suala la mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja ni kubwa sana," amesema Papa na kusisitiza kuwa wale wote wanaohusika na mafunzo kwa makasisi wahakikishe kuwa wanafunzi wao "wamekomaa kibinaadamu na kihisia" kabla ya kuwapatia Sakramenti ya Upadre (upadrisho).

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم