MBWA WA BUSH AOMBOLEZA... ATOA HESHIMA ZA MWISHO

Mbwa Sully akiwa amelala karibu na jeneza lenye mwili wa George HW Bush


Mbwa aliyekuwa amepewa kazi ya kuwa msaidizi wa rais wa zamani wa Marekani George HW Bush amepigwa picha akionekana kuomboleza karibu na jeneza la kiongozi huyo.

Bw Bush, aliyehudumu kama rais wa 41 wa Marekani kati ya mwaka 1989 na 1993 alifariki dunia Ijumaa usiku akiwa na miaka 94.

Sully, mbwa wa jamii ya golden labrador, atasafiri pamoja na mwili wa marehemu kwenye ndege kutoka Texas  kwenda DC kwa ndege ya Air Force One - ambayo kwa muda imepewa jina Special Air Mission 41, kwa heshima ya rais huyo.

Mwili huo utarejeshwa Texas Jumatano.

Mbwa huyo wa jina Sully atasindikiza jeneza hilo muda wote.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527