MCHUNGAJI MSIGWA AACHIWA KWA DHAMANA KESI YA KUTISHIA KUUA


Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amepandishwa kizimbani leo Alhamis Septemba 28,2017 katika Mahakama ya Mwanzo Mjini Iringa kwa madai ya kumtusi na kutishia kumuua aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kitwiru, Baraka Kimata.

Mbali na Msigwa pia Diwani wa Viti Maalum, Selestina Johanes na dereva wa mbunge huyo, Godi Mwaluka wamepandishwa kizimbani kwa kosa hilo.

Akisoma shtaka hilo Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo, Rehema Mayagilo amesema kuwa mbunge huyo na washtakiwa hao wawili wanashtakiwa kwa madai ya kumtusi na kutishia kumuua diwani huyo.

Hakimu Mayagilo amesema kuwa Msigwa na wenzake walitenda kosa hilo jana saa nane mchana katika viunga vya Ofisi za Halimashauri ya Manispaa ya Iringa.

Baada ya kusomewa shtaka hilo Msigwa na wenzake wamepata dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktober 9 mwaka huu itakapotajwa tena.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم