KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI AONGOZA KIKAO CHA MASHAURIANO KUHUSU MAUDHUI NA KANUNI MPYA ZA HUDUMA YA UTANGAZAJI TANZANIA (TV, RADIO, BLOG, ONLINE TV)


Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii (Bloggers, Online Media) wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel (Katikati waliokaa), viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya kumalizika kwa kikao cha mashauriano na Wadau kuhusu huduma ya Utangazaji (Maudhui) na kanuni za maudhui mitandaoni leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Kanuni ziliizojadiliwa ni maudhui yanayorushwa na vituo vya utangazaji vya Redio na Televisheni n maudhui mitandaoni (Online Content) Jumla ya vyombo vya habari 76 vilishiriki kwenye kikao hicho.

Wadau wamepewa wiki moja kuwasiliasha maoni yao kwenye kamati ya mashauriano ili yajadiliwe na kufanyiwa kazi kwa lengo la kuboresh kanuni. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Wamiliki wa Wmiliki na wafanyakazi wa Vituo vya Televisheni na Radio wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole 
Gabriel (Katikati waliokaa), viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya kumalizika kwa kikao cha mashauriano na Wadau kuhusu  huduma ya Utangazaji (Maudhui) na kanuni za maudhui mitandaoni leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza kuhusu mambo mbalimbali waliyokubaliana katika kikao cha mashauriano na Wadau kuhusu huduma ya Utangazaji (Maudhui) na kanuni za maudhui mitandaoni leo  kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam

Wadau wa habari wakiwa katika kikao hicho



Meneja Mipango na Utafiti wa Sahara Media Group, Nathan Rwehabura akichangia mada wakati wa kikao hicho, ambapo pia alilalamikia ada kubwa inayotozwa kwa mwaka wamiliki wa vituo vya tv ambayo ni dola 25,000 sawa na sh mil 60 

Dina Chaali wa Channel Ten akitafakari jambo katika kikao hicho
Mkurugenzi mstaafu wa Utangazaji wa TCRA, Habby Gunze akifafanua jambo katika kiao hicho

Wakili wa Jamii Forum Benedict akichangia mada wakati wa kikao hicho

Mkuu wa Vipindi wa EAST AFRICA radio, Nasser Kingu akichangia mada wakati wa kikao


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم