CCM YAFUTA UCHAGUZI WA WENYEVITI WA WILAYA NNE

Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (NEC), umefuta uchaguzi wa wenyeviti katika wilaya nne baada ya kubaini wagombea waliojitokeza hawakuwa na sifa.


Akitangaza uamuzi huo leo , Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, amezitaja wilaya hizo zilizofutiwa uchaguzi kwamba ni Moshi Mjini, Siha, Hai, pamoja na Makete.

Amesema sababu ya kufuta matokeo hayo ni kubainika kwamba wagombea waliojitokea hawakuwa na sifa, pamoja na kubainika kuwepo na viashiria hatarishi kwa chama.

Hivyo kutokana na uamuzi huo Polepole amesema kwamba wilaya hizo zitaanza upya mchakato wa uchaguzi huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم