BODI YA WADHAMINI YA SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) YATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA KATAVI


Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi ,George Waitara akisalimiana na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi ,Izumbe Msindai baada ya kuwasili na wajumbe wa Bodi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mtango Mtahiko akizungumza mara baada ya kuwapokea wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA . 
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi,Izumbe Msindai akieleza jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA wakati wakitembelea hifadhi hiyo. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi ,George Waitara akitizama Viboko katika hifadhi hiyo. 
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakichukua taswira ya viboko katika Hifadhi ya taifa ya Katavi walipotembelea .
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali Mstaafu ,George Waitara akizungumza na askari waliopo katika mafunzo ya awali ya Uhifadhi katika kambi ya mafunzo ya Mlele iliyopo mkoani Katavi.
Askari waliopo katika mafunzo ya awali ya Uhifadhi katika kambi ya mafunzo ya Mlele iliyopo mkoani Katavi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali Mstaafu ,George Waitara alipowatembelea.

******

Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikiongozwa na Mwenyekiti wa bodi Jenerali Mstaafu George Waitara imetembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa ajili ya kukagua utendaji kazi ambapo ilipata fursa ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Hifadhi Izumbe Msindai.

Bodi imepongeza utendaji kazi katika Hifadhi ya Katavi hususani suala zima la kupambana na ujangili na juhudi zinazofanywa katika kuongeza idadi ya watalii hifadhini.

Aidha, Jenerali Waitara aliutaka uongozi wa hifadhi kuongeza jitihada katika kukabiliana na changamoto za mifugo ambayo ni kubwa kwa Katavi na pia alipongeza uongozi wa mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali mstaafu Raphael Muhuga kwa ushirikiano mkubwa anaotoa kwa hifadhi katika kupambana na mifugo hifadhini.

Mapema kabla, bodi iliweza kutembelea kituo cha mafunzo cha Mlele na kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Kituo Mhifadhi Genes Shayo na kupata nafasi ya kuongea na askari wapya wanaoendelea na mafunzo katika kituo hicho.

Jenerali Waitara aliwataka askari hao kuwa na nidhamu, uwajibikaji, bidii na uzalendo katika mafunzo yao na kuwa ni lazima waonyeshe kuiva ili waweze kupambana vilivyo na changamoto ya ujangili katika Hifadhi za Taifa nchini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم