WAKILI WA TUNDU LISSU,FATMA KARUME AMBURUZA KORTINI ASKARI POLISI KWA KOSA LA KUMWINGILIA MWILINI NA KUMBUGHUDHI, ADAI FIDIA YA BILIONI MOJA

Wakili wa Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Fatma Karume amefungua kesi ya madai Mahakama Kuu ya Tanzania dhidi ya Inspekta wa Polisi Eugene Mwampondela wa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es salaam.


Fatma amesema kuwa Inspekta Mwampondela alimshika mkono na kumvuta kwa nguvu hali iliyomsababishia maumivu makali, hivyo anadai alipwe kiasi cha shilingi bilioni moja kwa kosa la kumwingilia mwilini mwake na kumbughudhi kwa kumzuia kufanya kazi yake.

“Aliniambia kuwa ameagizwa na wakubwa kutoka juu, hivyo namfikisha mahakamani ili amweleze jaji ni nani aliyemtuma, na mimi sitaki kushikwa shikwa mwili wangu kwa hiyo naomba anilipe shilingi bilioni moja ili liwe fundisho kwa wengine,”amesema Fatma.

Fatma ambaye ni mmoja wa mawakili wa Mbunge wa Singida Mashariki alikumbana na kadhia hiyo wakati akiwa katika harakati za kumtetea mteja wake ili aweze kupata dhamana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم