Makubwa Haya!! MWANAUME AOA MWANAUME MWENZIE BILA KUJUA HUKO MTWARA


Dunia imekwisha ndivyo unavyoweza kusema!! Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni...Kutoka Mkoani Mtwara tumepata habari kuwa mwanamme mmoja amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuoa mwanamme mwenzake bila kujua.

Hii imetokea katika Kijiji cha Mkahara, halmashauri ya mji wa Nanyamba, wilaya ya Mtwara, mkoani Mtwara ambapo mwanamme huyo amejikuta akivunja ukimya kuwa mtu aliyemuoa siyo mwanamke bali ni mwanamme kwani tangu amuoe takribani miezi minne hajawahi kufanya naye tendo la ndoa.

Tukio hilo limetokea baada ya mwanaume kukosea namba na kumpigia aliyejifanya mwanamke kisha kuanzisha uhusiano ya kimapenzi hata wakafikia hatua ya kukubaliana kufunga ndoa ambapo mwanaume huyo alikuwa anavaa mavazi ya kike kiasi kwamba ilikuwa ngumu kubainika kama ni mwanaume. 

Inaelezwa kuwa jamaa huyo kaishi na mwanamme mwenzie kwa muda wa miezi minne na kila akitaka wafanye tendo la ndoa mwenzie hudai kuwa anaumwa na kwamba shughuli zote zinazofanywa na akina mama nyumbani ikiwemo kuosha vyombo,kujipodoa,kupika anafanya vizuri tu.

Msikilize hapa mama mkwe akifunguka

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم