Picha: Nape Nnauye Aungana na Watanzania Wengine Kupokea Mwili wa Senga Aliyepiga Picha za Mauaji ya Mwangosi




Moja ya habari iliyotawala Julai 28 2016 katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari ilikuwa ni pamoja na hii ya kutokea nchini India iliyohusu kifo cha mpiga picha wa Gazeti la Tanzania Daima Joseph Senga aliyefariki akiwa katika matibabu ya ugonjwa wa moyo.




Marehemu Joseph Senga ndiye mpiga picha aliyenasa tukio la mauaji ya Mwandishi wa habari wa kituo cha talevisheni CHANEL 10 Daud Mwangosi kilichotokea September 2 2012 katika kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.



Leo Julai 30 2016 mwili wa marehemu Joseph Senga tayari umewasili nchini ukitokea India, ambapo Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye aliungana na baadhi ya watanzania wakiwemo wapiga picha wenzake wa kutokea vyombo mbalimbali vya habari.

Tayari nimekusogezea picha kutokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam 


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, (watatu kushoto), mbunge wa Nsumve Richard Ndasa, (wanne kushoto) na baadhi ya waandishi wa habari na wapiga picha, wakilitazama jeneza lenye mwili wa Joseph Senga, aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, wakati wafanyakazi wa Swissport wakilitoa jeneza hilo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2016 ulipowasili kutoka nchini India.



Waziri Nape Nnauye na wananchi wakishiriki kubeba jeneza






Baadhi ya wapiga picha wakiongozwa na Loveness Bernard wakiwa katika vazi la pamoja


Wapiga picha kutokea vyombo mbalimbali vya habari walipokuwa wakiusubiri mwili wa marehemu


Ndugu wa karibu akitokwa na machozi baada ya kuona jeneza lililobeba mwili wa marehemu Senga likiwasili

Waombolezaji wakisubiri mwaili kuwasili kutoka nchini India, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu tayari kwa safari ya kutoka uwanjani hapo kuelekea Muhimbili kuhifadhiwa


 
Othmani Michuzi,(kulia). wa Blog ya Mtaa kwa Mtaa, akimfariji mpiga picha wa Tanzania Daima, Loveness Bernard ambaye alifanya kazi ofisi moja na marehemu Senga

Baadhi ya wapiga picha na waombolezaji wengine wakiondoka baada ya mwili kuwasili

Mbunge wa Nsumve, Richard Ndasa, (kushoto) akimsikiliza aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Serikali, Daily News na Habari Leo, Gabriel Nderumaki wakati wakisubiri mwili wa marehemu Senga kuwasili
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia), akiteta jambo na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena, wakati wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu Joseph Senga, aliyekuwa mpiga picha mkuu wa gazeti hilo
Gari lililobeba jeneza lenye mwili wa marehemu Senga, likiwa tayari kuondoka uwanjani hapo

Msafara wa magari ukiwa tayari kuondoka
 (Picha zote na Othman Michuzi na Khalfan Said)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم