Watu 8 Wauawa Kwa Kuchinjwa Huko Tanga



Watu 8 wamechinjwa na miili yao kutenganishwa na vichwa akiwemo mjumbe wa serikali ya mtaa kufuatia vikundi vya uhalifu kuvamia nyumba za wakazi wa mtaa Kibatini uliopo kata ya Mzizima jijini Tanga hatua ambayo imeleta hofu kubwa kwa wananchi wa maeneo hayo. 

Wakizungumza katika eneo la tukio baadhi ya waathirika ambao ndugu jamaa na zao wamechinjwa majira ya saa saba usiku wamesema kundi la watuhumiwa wanaokadiriwa kuwa walikuwa watu nane na kuvalia nguo nyeusi walipofika katika nyumba zao waliwaamuru akina baba watoke nje kisha kuwapeleka hadi katika vichaka kisha kuwachinja. 


Tukio hilo limekuja wiki mbili tu baada ya vikundi hivyo vya uhalifu vinavyodaiwa kujificha katika mapango ya Amboni Mleni Maji moto kuchinja mbuzi 48,ng'ombe wawili na kuku zaidi ya 12 lakini Kamanda wa Polisi amekiri kuwa tukio hilo ni kubwa na kwamba jitihada za polisi zinafanywa ili kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanakamatwa na kutiwa mbaroni. 

Hata hivyo ndugu wa mjumbe wa serikali ya mtaa wa Kibatini ambaye naye ni miongoni mwa waliochinjwa amesema chanzo cha kundi hilo kuwafanyia unyama huo inatokana na kukamatwa kwa watoto wa watuhumiwa ambao ndio waliokuwa wakitumwa kabla makundi hayo hayafanya uhalifu.
Chanzo-ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم