Rais Magufuli Afanyiwa Ibada Maalum Ya Kimila na Viongozi wa Juu wa Kabila la Kimaasai



Zaidi ya viongozi mia moja wa mila kutoka kabila la maasai kwenye wilaya za watu wa jamii hiyo wamekusanyika wilayani Monduli mkoani Arusha kumsimika Kiongozi Mkuu wa mila wa koo ya Ilikisongo na kufanya ibada maalum ya kimila ya kumwombea Rais Magufuli na serikali yake waendelee kupambana na wafujaji wa mali ya umma. 
 
 
Katika tukio ilo lililohudhuriwa na viongozi wa mila kutoka wilaya za mikoa ya Arusha, Manyara, Morogoro na kwingineko pamoja baadhi ya viongozi wa kisiasa ambapo wengi wao ni wa jamii hiyo viongozi wa mila wamesema wapo tayari kushirikiana na serikali katika kuwafichua watendaji wazembe na wauza ardhi ya umma ili kuwaondoa watanzania kwenye dimbwi la umasikini. 
 

Kiongozi aliyesimikwa kama mwenyekiti wa viongozi wa mila wa koo hiyo Kibori Ngelipoi ,akizungumza huku akitafsiriwa kwakuwa hajui lugha ya kiswahili amesema nafasi ya viongozi wa mila katika jamii ni kubwa naye atahakikisha atatumia vizuri nafasi hiyo. 
 

Baadhi ya viongozi wa kisiasa waliohudhuria tukio hilo wamewaasa viongozi wa mila kutochanganya siasa na mila kwa kuwa vitashusha ufanisi wao katika kutatua masuala ya kijamii.
 
Chanzo-ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم