Jamaa Ang'atwa na NYOKA Kwenye UUME Wake Akijisaidia Chooni


Raia mmoja wa Thailand anaendelea kuuuguza jeraha katika hospitali moja baada ya nyoka aina ya chatu kutokea ndani ya choo na kumng'ata uume wake.


Attaporn Boonmakchuay,ambaye alipoteza damu nyingi amesema kuwa nyoka hiyo ilikuwa ikimvuta baada ya yeye na mkewe kujaribu kuipiga.

Madaktari wanasema kuwa Bw Attaporn ambaye alipoteza damu nyingi anaendelea vyema na matibabu.

Nyoka akitolewa katika choo hicho

Wafanyikazi walilazimka kukiharibu choo hicho.Baadaye nyoka huyo aliachiliwa na kuingia msituni.

Kisa hucho kilitokea wakati ambapo Attaporn mwenye umri wa miaka 38 alielekea katika choo chake nyumbani kwake huko Chachoengsao,mashariki mwa Bangkok kabla ya kwenda kazini siku ya Jumatano.

Wakati alipokuwa akitumia choo hicho alihisi uchungu mkali.

Nyoka aina ya chatu

''Nilihisi kama ambaye uume wangu ulikuwa umekatwa,Nyoka huyo alikuwa akinivuta kwa kutumia nguvu nyingi'',alisema.


Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم