|
Mwenyekiti wa BAVICHA taifa Patrobas Katambi
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo(BAVICHA) taifa Patrobas Katambi ametangaza kuwania ubunge wa jimbo la
Shinyanga Mjini Kupitia UKAWA katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Katambi ametangaza nia hiyo jana jioni wakati wa mkutano wa hadhara
uliofanyika katika viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Nguzo nane Mjini
Shinyanga,mkutano ambao umehudhuriwa na mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless
Lema.
Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa BAVICHA Katambi
alisema yeye ni mzaliwa wa Shinyanga hivyo atakomaa katika jimbo la Shinyanga
Mjini kuhakikisha anagombea ubunge ili kuondoa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi
ambao umekuwa ukifanya ubadhirifu wa fedha na kutowaletea maendeleo wananchi.
“Mimi ni mtu wa Shinyanga,Natangaza rasmi kuwa nitagombea
ubunge katika jimbo la Shinyanga Mjini,uwezo ninao na nia ninayo,naungana na
watangaza nia wengine waliotangulia,naomba ushirikiano tu,kama jina langu
litapitishwa tutafanya mambo makubwa katika jimbo hili”,alieleza Katambi.
Alisema endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo
nitakuwa mbunge wa Vitendo siyo maneno kama wanavyofanya wabunge wa CCM hasa
katika jimbo la Shinyanga ambao kazi yao ni kuongea tu na kula pesa za jimbo ba
kuwaacha wananchi wakiendelea kuwa maskini kila kukicha.
Nilirekodi Hotuba yake ya Kutangaza nia ,SIKILIZA HAPA CHINI
|
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553