Uchawi Morogoro!! NYUMBA ZAUNGUA KWA MOTO WA AJABU,WANANCHI WAHAHA,WALALA NJE SIKU 7 MFULULIZO


Katika hali  isiyo  kuwa  ya  kawaida  familia tatu zenye  watu  16  katika kijiji cha Mikese mkoani Morogoro wanalazimika  kulala nje kwa siku saba mfululizo baada  ya nyumba wanazoishi  kuwaka moto  mara kwa mara na kuunguza samani  za ndani  na  vyakula.


 Inaelezwa kuwa chanzo cha moto huo hakifamahamiki   na hivyo kusababisha   hofu kwa familia hizo kutaka kuyakimbia makazi yao.

Mwandishi wa habari hizi amefika katika familia hizo na kuona vitu mbalimbali vilivyoungua moto vikiwemo vyakula nguo madaftari ya wanafunzi  huku wakinamama na watoto  pamoja na wazee  wakiwa nje.

Wananchi hao wamesema katika hali isiyokuwa ya kawaidia moto huo huwaka  zaidi ya mara tisa kwa siku na wanajaribu kuuzima  lakini chanzo cha moto huo hakieleweki  ingawa nyumba hizo hazina umeme wala nishati ya aina yoyote  inayosabaisha moto.

Wananchi hao wamefananisha tukio hilo kama la miujiza na kuomba watu wenye  imani  mbambali kufika na kufanya maombi katika nyumba hizo kwani wanateseka kwa kushindwa  kulala ndani.

Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Lukole  Ramadhani  Shaban amekiri  kuwepo kwa matukio ya moto  kuwaka katika nyumba hizo kwa siku saba mfululizo.

Amesema  siyo tukio la kawaida na jitihada wanazozifanya kama serikali ya kijiji  wameanza kuwatafuta  wachungaji na mashekhe ili   kusaidia kufanya maombi katika  nyumba hizo kwani familia hizo zinaishi katika mazingira magumu ya kulala nje kwa muda mrefu.

Via>>Itv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم