Bad News!! MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI AUA MWANAFUNZI MWENZAKE DARASANI HUKO SHINYANGA VIJIJINI

Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Ilola iliyopo katika wilaya ya Shinyanga vijijini aitwaye Veronica Venance mwenye umri wa miaka 12 amefariki dunia kwa kupigwa na mwanafunzi mwenzake wakati wakigombania daftari darasani kwa ajili ya kuandika notes.


Walioshuhudia tukio hilo wamesema limetokea Februari 24 mwaka huu,  saa 7 na nusu mchana katika darasa la tano shule ya msingi Ilola iliyopo katika kata ya Ilola tarafa ya Itwangi wilaya ya Shinyanga.

Mshuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa mwanafunzi huyo amefariki dunia baada ya kupigwa makofi na ngumi sehemu za kichwani na mwanafunzi mwenzake aitwaye Sophia Mathew(12).


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527