Hii Kali!! MBWA MSTAAFU WA POLISI AAGWA KISHUJAA, AANDALIWA GWARIDE NA KUPIGIWA SALUTI NA POLISI

police-dog-sultan2Mbwa mmoja wa Polisi huko New Jersey Marekani mwenye umri wa miaka nane aliyefanya kazi kwa miaka minne amelazimika kustaafu kutokana na afya yake kuwa mbaya.


Mbwa huyo wa Polisi ambaye anaitwa Judge amepewa heshima na kuagwa kishujaa, kaandaliwa na gwaride pamoja na kupigiwa saluti na Polisi tukio ambalo lilishuhudiwa pia watu wa haki za wanyama.
judge24n-11-webJudge alikuwa anastaafu kama mbwa wa Polisi huko West Deptford Township, ambapo alitakiwa kustaafu tangu mwaka 2013, kutokana na maradhi ya meno na pia afya yake ilianza kuzorota kwa kasi.

Tangu ameanza kuumwa 2013 hali ya afya yake haikuwahi kuwa nzuri, watu wa haki za wanyama waliona ni vizuri ‘astaafishwe’ na pia wakashauri aendelee kupatiwa matibabu katika Hospitali ya wanyama ya Swedesboro.
img-2764-1-2048x1152-20150223-160806-799
IMG_2746
Huu ni msafara wa gari zilizombeba mbwa huyo.
police-dog-sultan
judge24n-9-web
Tukio hilo sio geni sana kwa wenzetu, kuliwahi kuwa na story ya ishu ya mbwa mmoja wa Polisi ambaye alizikwa kwa heshima kama ambavyo huwa mazishi ya askari yanafanyika.Angalia picha hapa chini
Screen-Shot-2014-10-12-at-1.19.48-PM
Shughuli za mazishi ya mbwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527