ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 9 ZAPATIKANA WAKATI WA HARAMBEE YA KUCHANGIA MFUKO WA KUSHUGHULIKIA MAKABURI YA WAISLAM YA NGUZO NANE MJINI SHINYANGA

 
 
Makaburi ya waislam ya Nguzo Nane mjini shinyanga,japokuwa yamezungushiwa ukuta lakini katika baadhi ya maeneo hakujazibwa na kusababisha baadhi ya watu wanaoishi kando kando ya eneo hilo kutupa uchafu katika makaburi hayo ambapo ni wakati mzuri sasa kuachana na tabia hiyo kama walivyoeleza viongozi wa dini ya kiislam waliofika hapo jana wakati wa uzinduzi wa mfuko wa kushughulikia makaburi hayo

Wa pili kutoka kushoto ni mkuu wa mkoa wa shinyanga Ally Nassoro Rufunga akiwasili katika eneo la makaburi ya Nguzo nane mjini shinyanga hapo jana,tayari kwa uzinduzi wa mfuko wa kushughilikia makaburi hayo.Mkuu huyo wa mkoa alisema mfuko huo utasaidia sana kwani watu wasio na uwezo watazikwa bure huku wengine wakichangia kiasi flani.Mbali na hayo alipompongeza mbunge wa kishapu kwa kushiriki katika shughuli za kijamii kwani huo ndio upendo wa dhati kwa wananchi na jamii kwa ujumla.
 
Sheikh Nassoro Said Elmaamry kutoka Jumuiya ya East Qaama Tanzania akitoa neno wakati wa uzinduzi wa mfuko wa kushughulikia shughuli za makaburi ya Waislam ya Nguzo nane,ikiwa ni jitihada za mbunge wa jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Mheshimiwa Suleiman Nchambi kwa kushirikiana na viongozi wengine akiwemo sheikh mkuu wa mkoa wa shinyanga.Sheikh Nassoro alionesha kufurahia  kitendo cha mbunge huyo kushiriki kwa moyo mmoja katika shughuli za kijamii
Mbunge wa kishapu suleiman Nchambi akisoma taarifa kuhusu jengo maalum kwa ajili ya kushughulikia miili ya marehemu ambapo alisema katika eneo hilo taarifa mbalimbali za watu waliozikwa pale zitakuwepo,taarifa za misiba na mazishi zitapitia pale na usimamizi wa makaburi hayo lakini pia akieelezea kuhusu mfuko wa kushughulikia makaburi ya Nguzo nane ambapo alisema jamii inapaswa kujenga tabia ya kutembelea makaburi na kuyathamini

 
Sheikh mkuu wa mkoa akizungumzia kuhusu kifo kwamba kila mwanadamu lazima atapitia makaburini ikiwa ni njia ya kuelekea ahera yaani kwa mungu aliyetuumba hiyo tukiwa hai yatupasa kujiandaa kwa kutenda mema hapa duniani
 Hapa anawaeleza waumini wa dini ya kiislam umuhimu wa kutembelea makaburi kwamba mtu akitembelea makaburi anakuwa  anakumbuka ahera
 
Aliyevaa nguo nyeusi ni Mbunge wa Kishapu alifuatilia maneno kutoka kwa sheikh mkuu wa mkoa
 
Sheikh mkuu wa mkoa akihamasisha watu waliofika eneo hilo kuchangia mfuko uliozinduliwa ambapo zaidi sh milion 9 zilipatikana baada ya kufanyika kwa harambee hiyo,ambapo viongozi akiwemo mkuu wa mkoa wa shinyanga walichangia mfuko huo
 

  waumini wa dini ya kiislam wakifuatilia kilichokuwa kinaendela katika eneo hilo la makaburi

 Waumini wa dini ya kiislam wanafuatilia kinachoendelea
 
 Sheikh mkuu wa mkoa wa shinyanga Ismail Makusanya akionesha sanda ilifungwa tayari kutumika ambayo ni moja ya vitu vitakavyokuwa vinapatikana katika jengo maalum kwa ajili ya kuhifadhia na kuandaa maiti lililopo katika eneo la makaburi ya waislam ya Nguzo nane mjini Shinyanga,ambalo lilikuwa linatumika tangu mwanzo lakini kwa sasa limefanyiwa maboresho ya hali ya juu.Alisema sanda hizo zimetoka Karachi Pakistan.
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم