KATIBU MKUU TUGHE TAIFA ALLY KIWENGE AFANYA ZIARA YA GHAFLA SHINYANGA


 Katibu mkuu wa TUGHE taifa amefanya ziara ya siku mbili mkoani shinyanga na kuzungumza wa watumishi wa umma katika ukumbi wa NSSF uliopo mjini shinyanga kisha kuelekea katika hospitali ya mkoa huo na kuzungumza na madaktari ,manesi na wauguzi wa hospitali hiyo hapo jana leo yupo mkoani Simiyu akiendelea na ziara yake

Katibu mkuu wa wanachama wa Chama Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya Tanzania (TUGHE)Ally Kiwenge akiwa mkoani  Shinyanga,wakati wa ziara ya siku mbili ,akifuatilia kwa umakini na kuhuzunishwa na kero zinazowakabili wafanyakazi ikiwemo kucheleweshewa mishahara na kukatwa makatao bila ridhaa yao ,alipofanya kikao na wanachama hao katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga.


Ally Kiwenge akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwataka aliwataka waajiri baada ya kupokea malalamiko mengi dhidi yao ,kujichunguza na kuacha mara moja tabia ya kuwalazimisha wafanyakazi kufanya wanavyotaka wao kinyume cha sheria na maadili ya kazi huku pia akikemea tabia ya baadhi ya waajiri kuficha posho za wafanyakazi wao.


·         Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa shinyanga Dk Fredrick Mlekwa akifuatilia hotuba ya katibu mkuu TUGHE taifa  hapo jana ambapo alisema pamoja na mafanikio yaliyofikiwa na hospitali hiyo kama vile kupungua kwa idadi ya vifo kwa wagonjwa wanaolazwa,kupngua kwa vifo vya akina mama na watoto na kupungua kwa malalamiko ya wananchi,alizitaja  pia changamoto zinazoikabili hospitali hiyo kuwa ni pamoja na uhaba wa watumishi,ukosefu wa nyumba za watumishi ,upungufu wa dawa na ukosefu wa gari la kusafirishia watumishi
·          

Viongozi TUGHE mkoa wa Shinyanga

Kiwanga akizungumza na watumishi wa hospitali ya mkoa wa shinyanga

Watumishi wa hospitali ya mkoa wa shinyanga wakimsikliza katibu wao hospitalini hapo ambapo walieleza kukerwa na hali ya kucheleweshewa mishahara:PICHA ZOTE NA KADAMA MALUNDE

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم