Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MADHEHEBU YOTE KUKUTANA SHINYANGA KATIKA IBADA YA ‘NIMEBEBA USHUHUDA’




Na Elizabeth Cosmas - Shinyanga

Kwaya ya Vijana ya Kanisa la AIC Kambarage, maarufu kama Kambarage Vijana Choir (KVC), imewaalika waumini wa madhehebu mbalimbali na wananchi kwa ujumla kushiriki katika ibada maalum ya uimbaji itakayofanyika Ijumaa, Oktoba 16, 2026, katika Kanisa la AIC Kambarage, Manispaa ya Shinyanga.

Ibada hiyo yenye kaulimbiu ya “Nimebeba Ushuhuda” inalenga kuwaunganisha waumini katika kumwabudu Mungu pamoja na kuhamasisha amani, upendo na mshikamano ndani ya jamii.

Akizungumza kuhusu maandalizi ya ibada hiyo, Mwenyekiti wa KVC, Kheri Ndaki, amesema wameandaa tukio hilo kwa lengo la kutumia muziki wa Injili kuifikia jamii na kuimarisha umoja miongoni mwa waumini.

Amesisitiza kuwa ibada hiyo ni fursa kwa wananchi kutoka madhehebu mbalimbali kukutana na kushiriki pamoja katika kumsifu na kumwabudu Mungu.

KVC imewahimiza wananchi wa Shinyanga na maeneo mengine nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki ibada hiyo, huku ikisisitiza umuhimu wa kuendelea kudumisha amani, upendo na mshikamano kupitia imani na muziki wa Injili.


Mwenyekiti wa Kambarage Vijana Choir (KVC), Kheri Ndaki, akizungumza kuhusu maandalizi ya ibada maalum ya uimbaji ya “Nimebeba Ushuhuda” inayotarajiwa kufanyika Oktoba 16, 2026, katika Kanisa la AIC Kambarage, Manispaa ya Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com