TGNP YAZINDUA MRADI WA BORESHA HABARI KATIKA VYUO VYA UANDISHI WA HABARI KUHAMASISHA UANDISHI WENYE MRENGO WA KIJINSIA


Mratibu wa Mradi wa Boresha habari Mariam Oushoudada akitoa maelezo kuhusu mradi huo kwa wageni waalikwa pamoja na wanafunzi wa chuo cha Practical School of Journalism wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika leo kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Mtangazaji wa Clouds TV, Sakina Lyoka akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Boresha Habari wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani uliofanyika katika Chuo cha Practical School of Journalism kilichopo jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Deo Temba akiwasilisha mada kuhusu masuala ya usawa kijinsia kwa wanafunzi wa Chuo cha Practical School of Journalism kwenye uzinduzi wa mradi wa Boresha Habari uliofanyika katika chuo hicho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Esther William akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja pamoja na maswali yaliyokuwa yanaulizwa wakati wakati wa uzinduzi wa mradi wa Boresha Habari 
Mkufunzi kutoka Chuo cha Practical School of Journalism akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) kwa kuweza kuzindua mradi wa Boresha Habari.
Baadhi ya wanafunzi wakufuatilia mada kwenye uzinduzi wa mradi wa Boresha Habari

***
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umezindua mradi wa Boresha Habari katika vyuo vya uandishi wa habari kuhamasisha uandishi wenye mrengo wa kijinsia.

Akizungumza leo Jumatano Machi 8,2023 wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Boresha Habari kwenye  Chuo cha Practical School of Journalism, Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Deo Temba amesema TGNP inapenda kuona waandishi wa habari ambao bado hawajaingia kwenye vitendo wanaelewa vizuri masuala yote ya usawa wa Kijinsia pamoja na kujua uandishi wa habari wa Kijinsia pamoja na kuijua jamii kwa ukaribu zaidi hasa wanawake, vijana na Watu wenye ulemavu.


Pia amesema lengo ni kuona waandishi hao wanaandika makala au habari zinazohusiana na masuala yenye mrengo wa Kijinsia kwa kwa kuweka kwenye mitandao ya kijamii ili kuleta matokeo chanya kwenye jamii.


"Bila kuwa na waandishi wa habari wazuri wanaojua masuala ya usawa wa Kijinsia hatuwezi kuwa na maendeleo mazuri hivyo uzinduzi wa mradi huo kwenye Chuo cha Practical School of Journalism ili kuanza mafunzo kwenye chuo hicho yanayohusiana na Masuala yenye mrengo wa Kijinsia", amesema Temba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments