BABU WA MIAKA 80 MBARONI TUHUMA ZA KUMBAKA MJUKUU WAKE WA MIAKA 8


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi
**

Na Halima Khoya - Malunde 1 blog 
Mwanaume aitwaye Luhende Tugwa (80) Mkazi wa Kijiji cha Ihapa Kata ya Oldshinyanga Manispaa ya Shinyanga, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake wa darasa la kwanza jina (limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka (8) na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.

Tukio hilo limetokea Februari 8, 2023 saa nne asubuhi baada ya mwanafunzi huyo kutoka shule na kumkuta babu yake, huku bibi akiwa ameenda shambani ndipo mwanaume huyo aliamua kutumia fursa hiyo kufanya kitendo hicho cha ukatili kwa mjukuu wake.


Akisimulia kuhusu tukio hilo, bibi wa mjukuu aliyefanyiwa ukatili huo  amesema kuwa alikuwa shambani ambapo baada ya kurudi alimkuta mtoto anaumwa akamuuliza mbona uko hivyo akajibu amechomwa na mti sehemu za siri baada ya kumwangalia alikuta anatiririka damu ndipo alichukua jukumu la kumpeleka shuleni kwa mwalimu mkuu na kumwambia kuwa mtoto ameumia.


Baada ya mwalimu mkuu wa shule ya Old Shinyanga Judith Julias kumwangalia vizuri mtoto huyo alibaini kuwa amebakwa, ndipo alimwambia bibi huyo kuwa mtoto kabakwa, walichukua jukumu la kwenda zahanati ya Old Shinyanga, lakini walipewa rufaa ya kwenda hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga, pia mwalimu alitoa taarifa kwa afisa maendeleo diwani na afisa elimu.


Mwalimu mkuu wa shule hiyo amesema baada ya kuona mtoto amebakwa alimdadisi mtoto huyo ambapo alisema kuwa amefanyiwa kitendo hicho na babu yake baada ya kutoka shule nà kumkuta babu akiwa peke yake.

"Alipokuja hapa bibi wa mtoto na mtoto aliniambia amefanyiwa kitendo hicho wakati akitoka shule lakini baada ya kumhoji vizuri kuwa nani aliyemfanyia kitendo hicho alimtaja babu yake, katika shule yetu tunafanya jitihada za kuwalinda watoto pindi wakiwa shuleni na pindi wanapoondoka,kwa kweli kitendo hiki ni cha unyama hivyo tuwaombe jamii iwalinde watoto,"alisema mwalimu Julius.

Dkt. Jusitina Tizeba bingwa wa magonjwa ya watoto katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga alisema wamempokea mtoto akiwa na hali mbaya ambapo amempatia matibabu na kufikia sasa hivi anaendelea vizuri na maumivu yamepungua.


Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema vitendo hivyo vinatokana na kuporomoka kwa maadili kwenye jamii, hivyo anaitaka jamii iache kufanya vitendo kama hivyo iwe na hofu ya Mungu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments