Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HAKUNA MIILI ILIYOPATIKANA IKIELEA MTO RUVU- POLISI PWANI



Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limetoa wito kwa Jamii kupuuza taarifa ya madai ya kuokotwa kwa miili ya watu sita iliyokuwa ikielea katika Mto Ruvu, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani, likiwataka pia wanaosambaza taarifa hiyo ya uongo kuacha mara moja kwani zinaleta taharuki kwa jamii.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Salim Morcase katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Jumanne Juni 09, 2026 amesema Polisi tayari wameanza kushughulikia suala hilo ili kuchunguza na kubaini chanzo chake na kwa atakayebainika, hatua kalu za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

"Kwa mara ya kwanza taarifa hiyo ilisambazwa tarehe 21.12.2016 na kutolewa ufafanuzi na aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna Robert Boaz. Pia tarehe 13.09.2025 taarifa hiyo ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na ufafanuzi kuhusu ukweli wa taarifa hiyo ulitolewa tarehe 14.09.2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani. Hata hivyo tarehe 08.06.2026 taarifa hiyo imeendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii japokuwa ufafanuzi ulishatolewa mara mbili kuwa taarifa hiyo sio ya kweli." Imesema Taarifa ya Kamanda Morcase.

Kulingana na Kamanda Morcase, taarifa hizo zimekuwa zikisambazwa zaidi katika mitandao ya Instagram na Facebook.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com