MAKAMANDA WA POLISI WATANGAZA KIAMA KWA WEZI WA MAFUTA, VIFAA VYA UJENZI RELI YA KISASA 'SGR' ...VITU KIBAO VYAKAMATWA

Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Januari 11,2023 wakati akitoa taarifa kuhusu matokeo ya Operesheni ya kubaini na kukamata wezi wa mafuta na vifaa vya ujenzi kwenye mradi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka - Mwanza. 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa akielezea hatua zinazochukuliwa na Makamanda wa Polisi Mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mwanza katika kulinda Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Isaka- Mwanza. Wa kwanza kushoto ni  Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta akifuatiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu ACP Blasius Chatanda na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa akiongozana na makamanda wa Polisi mikoa ya Shinyanga na Simiyu, Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta na maafisa mbalimbali wa jeshi la Polisi katika kituo cha Seke Stesheni kilichopo Malampaka Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Makamanda wa Polisi Mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mwanza wametoa onyo kali kwa watu wanaohujumu Ujenzi wa Mradi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Isaka hadi Mwanza kwa kuiba mafuta ya dizeli na vifaa vya ujenzi wakisisitiza kuwa ni lazima mradi huo uwe salama muda wote.

Onyo hilo limetolewa leo Jumatano Januari 11,2023 na Makamanda wa Polisi Mikoa ya Shinyanga (ACP Janeth Magomi), Simiyu (ACP Blasius Chatanda), na Mwanza (SACP Wilbroad Mutafungwa) walipotembelea Kambi Kuu ya Mkandarasi wa Kampuni ya ujenzi CCECC kwenye kituo cha Seke Stesheni kilichopo Malampaka Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu ili kupata taarifa kuhusu maendeleo ya mradi.
Akizungumza kwa niaba ya Makamanda wa Polisi Mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa amesema kamwe hawapo tayari kuona mradi huo unahujumiwa na baadhi ya wafanyakazi waliopo ndani ya mradi huo na wananchi walio nje ya mradi huo.

Kamanda Mutafungwa amesema Jeshi la Polisi katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mwanza wanaendelea na msako mkali na Operesheni ya Pamoja ‘Joint Operation’ ya kuwabaini na kuwakamata watu wote wanaohujumu ujenzi wa mradi huo wa Reli ya Kisasa kwa namna yoyote iwe kuiba,kupokea, kushiriki kuiba mafuta na vifaa vingine vya ujenzi.
Naibu Mkurugenzi wa Mradi wa SGR (Isaka – Mwanza) upande wa Mkandarasi Kampuni ya CCECC – CRCC JV, Bw. Wang Chao.

“Operesheni hii ni endelevu, tutahakikisha tunawakamata watu wote waliopo ndani ya mradi na walio nje ya mradi ambao kwa namna yoyot wanafanya uhalifu kwa kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi. Tunaomba wananchi endeleeni kushirikiana na Polisi kutupa taarifa fiche, na tayari tumekamata baadhi ya wahalifu,madumu,baiskeli na pikipiki wanazotumia kuiba”,amesema Mutafungwa.

“Huu ni Mradi Mkubwa sana na ni mali ya Watanzania wote, hivyo ni lazima kila mmoja ashiriki kuulinda. Tutatumia nguvu zote kuulinda, tunatuma salamu kwa wahalifu wakafute kazi nyingine ya kufanya siyo kuhujumu mradi huu. Tupeni taarifa tushughulike na wahalifu”,ameongeza Kamanda Mutafungwa.

Kamanda huyo wa Polisi Mwanza ametumia fursa hiyo kuyatahadharisha baadhi ya Makampuni ya Ulinzi yanayofanya kazi ya ulinzi kwenye mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kuzingatia maadili na uadilifu .

“Tunafuatilia pia kuhusu Makampuni ya ulinzi yenye ulegevu, haiwezekani vifaa vya ujenzi viibiwe Site. Sisi tunafuatilia pia, tupeni taarifa ili tufanye mapitio ya maadili na uadilifu. Pia tuendelee kutoa elimu kwa wananchi kwenye kata zote ambako mradi huu unapita,huko kuna Mkaguzi wa kata, tunataka wananchi wawe wamiliki wa mradi, waulinde”, amesema Mutafungwa.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema Makamanda wa Polisi wataendelea kushirikiana katika Operesheni ya kuwabaini na kuwakamata wahalifu wote ili mafuta na vifaa vya ujenzi visiibiwe kwa kupambana na baadhi ya wafanyakazi waliopo ndani ya mradi na waliopo nje ya mradi wanaoshirikiana katika wizi huo.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Blasius Chatanda amesema ana furahi kuona wimbi la wizi wa mafuta na vifaa vya ujenzi limepungua ukilinganisha na siku za mwanzo wakati ujenzi unaanza mnamo mwaka 2021.

“Nafurahi kuona wimbi la wizi limepungua, mwanzo hali ilikuwa mbaya, kulikuwa na udokozi uliohusisha wafanyakazi ndani ya mradi na waliopo nje ya mradi. Hali hiyo tumeidhibiti wamebaki wachache walio nje ya mradi ambao ni rahisi kupambana nao. Tuendelee kupeana taarifa na kushirikiana, haiwezekani mradi uhujumiwe na sisi tupo”,amesema Chatanda.

Naibu Mkurugenzi wa Mradi wa SGR (Isaka – Mwanza) upande wa Mkandarasi Kampuni ya CCECC – CRCC JV, Bw. Wang Chao, Mwanasheria wa Mradi Akida Majenga na Meneja Usalama wa Mradi huo, Wilbert Sichome wamesema licha ya maendeleo mazuri ya mradi, changamoto iliyopo ni udokozi wa mafuta na vifaa ambapo vifaa vimekuwa vikiibiwa Site na vibaka huku wakiomba kuwepo kwa magari ya doria ili kuimarisha hasa wanapoelekea kuongeza vifaa.
Madumu, mipira, baiskeli, pikipiki zilizokamatwa zikitumika kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi

Naye Afisa Rasilimali kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), Cornel Kyai amesema hali ya wizi wa vifaa vya ujenzi imepungua huku akiipongeza Operesheni inayoendelea kufanywa na Kikosi cha Polisi Reli na Jeshi la Polisi kuendelea kudhibiti vitendo vya wizi ambapo mpaka sasa mafuta zaidi ya lita 10,000 yameokolewa,pikipiki,baiskeli na watuhumiwa wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Akizungumzia matokeo ya Oparesheni inayoendelea, Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta amesema
tarehe 9 Januari 2023 majira ya saa 10:50 jioni katika eneo la Seke kwenye barabara ya mradi wa ujenzi wa reli wakiwa kwenye doria na misako ya wahalifu walimkamata Abel Luekila (22) mkazi wa Ngudu Kwimba akiwa na amepakia madumu 9 ya mafuta ya dizeli kwenye pikipiki aina ya Kinglion isiyo na usajili ambapo kila dumu la mafuta lilikuwa na ujazo wa lita 20 jumla lita 180.

Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta.

“Kwa kipindi cha mwezi mmoja hadi sasa jumla ya mafuta ya dizeli lita 520, ukiongeza lita 180 na kufanya idadi kuwa lita 700 yameokolewa na askari polisi wa reli ambapo wahalifu waliyaficha mafuta hayo kwenye vichaka”, ameeleza Mbuta.

“Vitu vingine vilivyotelekezwa na wahalifu kwa lengo la kukwepa mkono wa sheria ni pamoja na pikipiki zaidi ya 20, baiskeli 8, madumu tupu zaidi ya 120 yatumikayo na wahalifu kuiba mafuta na mipira 22 ya kunyonyea mafuta”,ameeleza Mbuta.

Amefananua kuwa kwa kipindi cha Mwezi Januari hadi Novemba 2021 walifanikiwa kukamata lita za mafuta 5820 yenye thamani ya shilingi 18,328,870/=.

“Kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Novemba 2022 tulikamata mafuta ya dizeli lita 13,922 yenye thamani ya shilingi 43,589,782/= ambapo thamani ya mafuta yote ni shilingi 61,918,652/=. Hii ni thamani ya mafuta kabla ya matukio mapya. Tayari watu 21 wamefungwa jela”,amesema.

“Tumejipanga vizuri, hakuna mhalifu atabaki salama. Kwa yeyote atakayeingiwa na tamaa ya kuiba vifaa vya ujenzi, mafuta tutamfikia popote alipo, tutamkamata na kumfikisha mahakamani., kikubwa tuendelee kupeana taarifa”,amesema Mbuta.

“Mradi huu wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ni wetu Watanzania hivyo kila mmoja anatakiwa kuwa mlinzi wa reli hii, vifaa vinavyotumika na mafuta. Wenyeviti vitongoji, mitaa na viongozi wote kwa kushirikiana na wananchi kila mmoja anatakiwa kuwa mlinzi na kutoa ushirikiano wa hali ya juu kuhakikisha reli yetu muda wote inakuwa salama”, ameongeza Mbuta.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa akizungumza kwenye kituo cha Seke Stesheni kilichopo Malampaka Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu leo Jumatano Januari 11,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa akizungumza kwenye kituo cha Seke Stesheni kilichopo Malampaka Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Januari 1,2023 wakati akitoa taarifa kuhusu matokeo ya Operesheni ya kubaini na kukamata wezi wa mafuta na vifaa vya ujenzi kwenye mradi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka - Mwanza. 
Maafisa wa Polisi wakiwa katika kituo cha Seke Stesheni
Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta akionesha madumu, baiskeli, pikipiki, mipira iliyokamatwa ikitumika kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi kwenye mradi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka - Mwanza. 

Madumu, baiskeli, pikipiki, mipira iliyokamatwa ikitumika kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi kwenye mradi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka - Mwanza. 
Madumu, baiskeli, pikipiki, mipira iliyokamatwa ikitumika kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi kwenye mradi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka - Mwanza. 
Sehemu ya madumu, baiskeli, pikipiki, mipira iliyokamatwa ikitumika kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi kwenye mradi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka - Mwanza. 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa (kushoto)  akizungumza na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta, Makamanda wa Polisi na maafisa wa polisi Mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mwanza namna ya kulinda Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Isaka- Mwanza.
Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta,  akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) 

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu ACP Blasius Chatanda akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
Naibu Mkurugenzi wa Mradi wa SGR (Isaka – Mwanza) upande wa Mkandarasi Kampuni ya CCECC – CRCC JV, Bw. Wang Chao akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
Meneja Usalama wa Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka- Mwanza Wilbert Sichome akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
Meneja Usalama wa Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka- Mwanza Wilbert Sichome (kushoto) akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
Mwanasheria wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Akida Majenga akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)

Afisa Rasilimali kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), Cornel Kyai 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa akiongozana na makamanda wa Polisi mikoa ya Shinyanga na Simiyu, Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta na maafisa mbalimbali wa jeshi la Polisi katika kituo cha Seke Stesheni kilichopo Malampaka Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments