NIDA YATAMBULISHA MFUMO MPYA WA USAJILI KWA NJIA YA MTANDAO

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bw.Geofrey Tengeneza (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Meneja Usajili na Utambuzi (NIDA), Bi.Julien Mafuru na kushoto kwake ni Kaimu Mkuu Uratibu Ofisi za Wilaya NIDA, Bi.Brenda Kileo. Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bw.Geofrey Tengeneza (katikati) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Meneja Usajili na Utambuzi (NIDA), Bi.Julien Mafuru na kushoto kwake ni Kaimu Mkuu Uratibu Ofisi za Wilaya NIDA, Bi.Brenda Kileo. Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bw.Geofrey Tengeneza (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 21,2022 katika ofisi za NIDA Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bw.Geofrey Tengeneza (katikati) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 21,2022 katika ofisi za NIDA Jijini Dar es Salaam, Meneja Usajili na Utambuzi (NIDA), Bi.Julien Mafuru akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 21,2022 katika ofisi za NIDA Jijini Dar es Salaam,

***********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetambulisha Mfumo wa Usajili wa Watu kwa njia ya mtandao utakaowezesha wananchi wenye sifa za kuomba Vitambulisho vya Taifa kwa kujaza fomu mtandaoni mahali popote bila kulazimika kufika katika Ofisi za NIDA.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Desemba 21, 2022 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (NIDA) Bw.Geofrey Tengeneza amesema ili kujisajili mwombaji ataandika eonline.nida.go.tz katika mtandao wa internet na kufuata maelekezo.

"Mfumo huu unalenga kupunguza usumbufu kwa waombaji wa Vitambulisho vya Taifa ambao kwa sasa wanalazimika kufika ofisi za NIDA kuchukua fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa kwani kupitia mfumo huu ujazaji wa fomu na kuweka viambatisho utafanyika mahali popote kwa kutumia kifaa chenye uwezo wa kupokea mtandao wa mawasiliano". Amesema Bw.Tengeneza.

Amesema baadda ya kujaza fomu, mwombaji atatakiwa kuchapa fomu (print)na kuipeleka fomu yake ofisi za NIDA iliyoko katika Wilaya anayoishi akiwa na nakala ngumu za viambatisho alivyopakia katika mfumo ili kukamilisha utaratibu wa usajili kama vile kuhojiwa na Uhamiaji, kupigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole.

Aidha amesema kuwa mfumo huo utapunguza muda unaotumika katika kusajili taarifa za mwombaji kwa kuwa usajili wa taarifa za mwombaji utakuwa umefanywa na mwombaji mwenyewe.

"Pamoja na kurahisisha huduma ya usajili kwa raia na wageni wakaazi, utapunguza pia gharama zinazotumika katika kuchapisha fomu za usajili na gharama za uchakataji wa taarifa". Amesema.

Hata hivyo amesema kuwa usajili kwa njia ya mtandao utaongeza idadi ya watu wanaojisajili kwa kuwa huduma hiyo itapatikana mahali popote badala ya kufika katika ofisi ya NIDA kufuata huduma hiyo.

Kwa upande wake Meneja Usajili na Utambuzi (NIDA), Bi.Julien Mafuru amesema kumekuwa na malalamiko ya kukosewa kwa taarifa za uombaji vitambulisho hivyo kupitia mfumo huu utasaidia kupunguza kero hiyo kwani mwombaji atajaza taarifa zake mwenyewe.

Amesema wanaenda kupanua wigo wa kuwaandikisha watanzania ambao watakuwa nje ya nchi kwahiyo na wenyewe watapata faida ya kujaza foma moja kwa moja kwenye mtandao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments