TETEMEKO LA ARDHI LAUA WATU ZAIDI YA 40 INDONESIA


Tetemeko la ardhi limekikumba kisiwa kikuu cha Indonesia cha Java na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 40 na mamia kujeruhiwa, wamesema maafisa wa eneo hilo wamethibitisha.


Tetemeko hilo lenye ukubwa wa kipimo cha richa 5.6 lilipiga mji wa Cianjur magharibi mwa Java, katika kina kirefu cha kilomita , kulingana na takwimu za Utafiti wa Jiolojia wa Marekani.

Tetemeko hilo lilisikika katika mji mkuu Jakarta umbali wa kilomita 100, ambako watu waliokuwa katika majengo marefu walihamishwa. Maafisa wanaonya juu ya uwezekano wa kutokea kwa matetemeko mengine huku idadi ya vifo ikitarajiwa kuongezeka.

Eneo ambalo tetemeko hilo lilitokea lina watu wengi na linakabiliwa na maporomoko ya ardhi, huku nyumba zilizojengwa sio imara. Waokoaji wamekuwa wakijaribu kuwahamisha watu kutoka kwenye majengo yaliyoporomoka, na kufanikiwa kumuokoa mwanamke na mtoto wake, kulingana na ripoti za eneo hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments