RAS NGUVILA : MKOA KAGERA TUTAPOTEZA SIFA KAMA TUTARUHUSU SWALA LA MAUAJI NA WATU KIJINYONGA




Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Mh. Toba Nguvila akizungumza
**
Na Mbuke Shilagi Kagera.

Katibu tawala Mkoa wa Kagera Mh. Toba Nguvila amewataka viongozi wa dini pamoja na Baraza la Amani Mkoani Kagera  kuuweka Mkoa huo madhabahuni na kuiombea jamii kuondokana na ibilisi anaye chafua Mkoa ambao kwa sasa umekithiri mauaji ya kujinyonga.

Akizungumza katika Ibada ya Kanisa la Kiinjili Tanzania KKKT Diyosis ya Kaskazini Magharibi Manispaa ya Bukoba amesema kuwa kwa sasa Ibilisi amekuja watu wamejisahau na kuchukua sheria mkononi na kuanza kuchinja watu kama ng'ombe na kusema kuwa jambo hilo halikubaliki.

"Tuna kazi ya msingi sana viongozi wa dini, viongozi wa Serikali tunayo Mabaraza ya Amani kwenye Mkoa, Wilaya na Kata lengo ni kuhakikisha kwamba jamii inakuwa na mtengo mzuri na utulivu sana",amesema Nguvila.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments