AMVIZIA KISHA KUMBAKA NA KUMUUA MKE WA RAFIKI YAKE AKIWA KAZINI


Polisi wanawazuilia wanaume wawili kuhusiana na mauaji ya mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 26 eneo la Mowlem, mtaani Umoja katika Kaunti ya Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), Edwin Onditi Odada (mshukiwa mkuu) na Samuel Juma Otieno walinaswa Jumatano, Julai 20, kuhusiana na kifo cha Pamela Asesa.

 Ripoti ya DCI inasema kuwa Odada ambaye ni rafiki wa karibu wa mume wa mwendazake, alibisha kwa nyumba ya wawili hao na Pamela kumkaribisha huku mumewe ambaye ni mhandisi katika kampuni moja kwenye barabara ya Mombasa jijini Nairobi akiwa kazini.


Mshukiwa mkuu anaripotiwa kumbaka mke wa rafiki yake kabla ya kumuua kwa kumnyonga kutumia nguo ambayo pia aliijaza kwenye mdomo wa mwendazake kabla ya kufunga mlango na kutoroka.


Odada amekiri kutekeleza mauaji hayo mnamo Julai 12,2022 huku Otieno akiwa mshukiwa wa pili kwa kupatikana na simu ya mwendazake. 

Uchunguzi wa polisi unaonyesha kuwa mumewe alirejea nyumbani mwendo wa saa mbili usiku na kupata mlango wa nyumba yake umefungwa huku simu zake zikikosa kupokelewa.

 Alitiisha usaidizi na kuvunja mlango huo ambapo alipigwa na butwaa baada ya kupata mwili wa mkewe ukiwa kitandani na kitambaa mdomoni. 

Washukiwa walikamatwa eneo la Tushauriane mtaani Kayole wakitarajiwa kufikishwa mahakamani. Kabla ya tukio hilo, mwanamke huyo aliwahi kumwambia mumewe kuwa rafiki yake alijaribu kumbaka.

 Mshukiwa alikuwa rafiki wa karibu wa mume wa mhasiriwa kiasi kwamba walikuwa wakiishi pamoja katika nyumba hiyo. Oduor hata hivyo alimtimua mshukiwa baada ya kuarifiwa na mkewe kuwa alijaribu kumbaka kisha baadaye akarejea kutekeleza unyama huo.

Via > Tuko news

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments