RAIS SAMIA AWASIHI WATANZANIA KUENDELEZA FALSAFA ZA HAYATI MWALIMU NYERERE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Kanali Abdulrahman Kinana , wakiwasili katika viwanja vya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoani Pwani kwa ajili ya kuzungumza na Viongozi mbalimbali, Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Wananchi wa Mkoa wa Pwani, kwenye Mdahalo wa Kitaifa wa Kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali, wanafunzi wa Vyuo Vikuu na wananchi wa Pwani katika Mdahalo wa Kitaifa wa Kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoani Pwani.


SEHEMU ya Viongozi mbalimbali wakifatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali, wanafunzi wa Vyuo Vikuu na wananchi wa Pwani katika Mdahalo wa Kitaifa wa Kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoani Pwani



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua Vitabu 3 vya Hayati Mwalimu Nyerere (Mwalimu Julius Kambarage Nyerere: Chemichemi ya fikra za Kimapinduzi, Misingi ya Falsafa, Itikadi na Sera za Chama cha Mapinduzi na Development as Rebellion-The Making of a Philosopher Ruler; Becoming Nationalist ; Rebelion without Rebels; katika Mdahalo wa Kumbukizi ya miaka 100 iliyofanyika Viwanja vya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoani Pwani


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionyesha vitabu mara baada ya kuzindua Vitabu 3 vya Hayati Mwalimu Nyerere (Mwalimu Julius Kambarage Nyerere: Chemichemi ya fikra za Kimapinduzi, Misingi ya Falsafa, Itikadi na Sera za Chama cha Mapinduzi na Development as Rebellion-The Making of a Philosopher Ruler; Becoming Nationalist ; Rebelion without Rebels; katika Mdahalo wa Kumbukizi ya miaka 100 iliyofanyika Viwanja vya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoani Pwani


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi tuzo Makongoro Nyerere mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyepokea kwa niaba ya Familia yake katika Kumbukizi ya miaka 100 iliyofanyika Viwanja vya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoani Pwani

...................................................

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi aliyekuwa na fikra na falsafa za dhana ya kujitegemea wakati wa uongozi wake.

Rais Samia amesema hayo leo wakati akihutubia katika Mdahalo wa Kitaifa wa kuadhimisha Miaka 100 ya Kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere.

Aidha, Rais Samia amesma Mwalimu Nyerere aliamini Tanzania na Mataifa mengine ya Afrika hayawezi kuwa na nguvu ya kuijiamulia mambo yake endapo yataendelea kuwa na uchumi tegemezi hivyo hatuna budi kuwajibika kwa kuchapa kazi na kutumia vizuri rasilimali tulizonazo ili tujitegemee kiuchumi.

Rais Samia amesema ili kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi, Serikali ya Awamu ya Sita inafanya jitihada mbalimbali kama kuimarisha huduma za afya, miundombinu ya elimu na viwango vya elimu.

Aidha, Rais Samia amemuelezea Mwalimu Nyerere kama kiongozi aliyejenga misingi imara ya amani, umoja, na mshikamano tuliyonayo hivi sasa ambayo inaendelezwa na kila awamu ya uongozi.

Rais Samia ametoa wito kwa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kuwa kitovu cha uandishi na uhifadhi wa historia ya harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika na maeneo yaliyohusishwa katika harakati za ukombozi yatambuliwe na kuendelezwa ili yatumike kama kivutio cha utalii wa kihistoria.

Katika maadhimisho hayo, Rais Samia alizindua vitabu vitatu ambavyo ni: Mwalimu Julius Kambarage Nyerere: Chemchemi ya Fira za Kimapinduzi; Misingi ya Falsafa, Itikadi na Sera za Chama Cha Mapinduzi na Development as Rebellion chenye Juzuu Tatu za The Making of a Philosopher Ruler, Becoming Nationalist na Rebellion without Rebels.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments