POLISI, MAHABUSU WAFARIKI KWA AJALI GEITA



Watu wanne ambao ni askari wa Jeshi la Polisi wawili na mahabusu wawili wamefariki dunia, kwenye ajali iliyotokea katika kijiji cha Ibanda mkoani Geita.

Ajali hiyo imetokea April 27 majira ya saa 10:00 jioni ikihusisha gari la Polisi namba PT 3798 Toyota Landcruiser lililokuwa likitokea Geita kusikiliza kesi mahakamani, kugongana na Lori aina ya Scania namba T 691 DBQ mali ya kampuni ya Nyanza lililokuwa likitokea mkoani Mwanza kuelekea mkoani Geita.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Henry Mwaibambe ameeleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni gari la Polisi kupata hitilafu.

Mganga Mfawidhi hospitali ya rufaa mkoa wa Geita Dkt. Mfaume Salum amesema alipokea majeruhi watatu na wote wamepatiwa matibabu mmoja anaweza kuruhusiwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments