MKONGWE WA VITA MWANZILISHI WA SEAL TEAM SIX AFARIKI DUNIA



Richard Marcinko, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 81, aliweka alama yake katika jeshi la Marekani kama kamanda mwanzilishi wa Seal Team Six, mojawapo ya vitengo vya vya mafunzo ya hali juu Marekani ambavyo baadaye vingefanya uvamizi hatari dhidi ya Osama Bin Laden.


Mkongwe wa Vita vya Vietnam, aliongoza kikundi hicho kwa miaka yake mitatu ya kwanza, na alitunukiwa zaidi ya medali 30 na nukuu wakati wa kazi yake na Jeshi la Wanamaji la Marekani.


Mtindo wake wa uongozi wa moja kwa moja na wa 'kimabavu' ulileta mafanikio makubwa lakini mara nyingi ulisababisha migogoro na wakubwa. Baadhi walimshutumu kwa kuhimiza utamaduni wa kutojali, "Kijana mbaya" katika Timu ya Seal Team .


Akiwa nje ya uwanja wa vita, Marcinko alikabiliwa na vita vya kisheria na alifungwa kwa muda mfupi kwa kulaghai serikali ya Marekani.


Licha ya hayo, alitekeleza jukumu muhimu katika kukuza uwezo wa Marekani wa kukabiliana na ugaidi katika kipindi cha mwisho cha Vita Baridi.


Sifa zake kubwa kuliko maisha ya kawaida , na wasifu wake Rogue Warrior, ulisaidia kuimarisha nafasi ya Kikosi cha Seal Team Six katika ngano za kijeshi na utamaduni ulioenea .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments