SERIKALI KUONGEZA UBUNIFU UTOAJI HUDUMA ZA POSTA NCHINI KURAHISISHA UTAMBUZI WA MAKAZI | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, October 7, 2021

SERIKALI KUONGEZA UBUNIFU UTOAJI HUDUMA ZA POSTA NCHINI KURAHISISHA UTAMBUZI WA MAKAZI

  Malunde       Thursday, October 7, 2021

Naibu Katibu Mkuu wa Habari, Mawasiliano na TEHAMA Dkt. Jim Yonazi   akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha ya watoa huduma za Posta nchini ikiwa ni wiki ya Posta Duniani.
Naibu Katibu Mkuu wa Habari, Mawasiliano na TEHAMA Dkt. Jim Yonazi   akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha ya watoa huduma za Posta nchini ikiwa ni wiki ya Posta Duniani.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Bakari akiongea kwenye warsha hiyo  ambao ameeleza TCRA ilivyojidhatiti  kuongeza wigo huduma za Posta kwa Jamii.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Bakari akiongea kwenye warsha hiyo  ambao ameeleza TCRA ilivyojidhatiti  kuongeza wigo huduma za Posta Kwa Jamii.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya watoa huduma za posta nchini wakisikiliza kwa makini masuala mbalimbali yanayohusu huduma za Posta.
***
Na Dotto Kwilasa, Dodoma

TANZANIA ikiwa inaadhimisha wiki ya Posta Duniani, Serikali imesema inaendelea kuongeza ubunifu katika kuboresha huduma za Posta nchini kuendana na ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia ikiwa ni pamoja na kuhakikisha nchi nzima inafikiwa na mfumo wa anuani za makazi kurahisisha utambuzi na utoaji huduma bora kwa jamii.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 7,2021,Jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu wa Habari, Mawasiliano na TEHAMA Dkt. Jim Yonazi wakati  akifungua warsha ya watoa huduma za Posta nchini ,huku akisisitiza kuwa ni muhimu kuleta ubunifu kuwezesha utoaji huduma na ufikishaji wa vifurushi na vipeto katika maeneo ya makazi, ofisi na sehemu za biashara.

 Aidha amesema ubunifu huo utasaidia pia utoaji wa huduma nyingine za jamii zikiwemo huduma za kutoa taarifa kwa zima moto na polisi .

 Akiongea kwenye warsha hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Yonazi amesema hadi sasa jumla ya Halmashauri ishirini na moja tayari zimefikiwa na huduma ya anuani za Makazi na kwamba kinachoendekea kwa sasa ni  kuunganisha  mfumo huo Kwa nchi nzima.

“Ili kuendelea kiuchumi lazima tutumie huduma za Posta nchini,kila mtu atambue umuhimu wake Katika kukuza uchumi wetu,faida kubwa ya posta  inawezesha bidhaa moja kutoka sehemu moja mpaka nyingine na usafirishaji wa mizigo bado unabaki kuwa ni kitu muhimu,"amesema.

Licha ya hayo ameeleza kuwa Serikali imeeneza  Postikodi katika Halmashauri 21 nchini na mipango inaendelea kuweka katika maeneo mengine hali itakayosaidia mizigo kufika kila mahali,kwa wakati na bila ubabaishaji.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Bakari amesema warsha hiyo ni muhimu kwani hutoa huduma   ya kusafirisha mizigo kwa umakini huku akisisitiza kuwa TCRA imejidhatiti kuhakikisha huduma za posta nchini  inakuwa ya  ushindani kwa shabaha ya kuongeza wigo  wa utoaji huduma badala ya kuachia huduma hizo kwa watumiaji wachache.

"Huduma za posta zilizoboreshwa ni muhimu kwa Maendeleo ya nchi, kwa kuzingatia kuwa  zinawezesha mabadilishano ya bidhaa za biashara zinazowezesha ukuaji wa uchumi wa Viwanda,lazima jamii itambue kuwa kuendesha biashara kidigitali ni nguzo kuu ya mabadiliko ya kiuchumi,"amesema.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post