AMUUA MME BAADA YA KULAZIMISHWA KUFANYA TENDO LA NDOA....ASEMA HAMPENDI, SIYO CHAGUO LAKE | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, April 15, 2021

AMUUA MME BAADA YA KULAZIMISHWA KUFANYA TENDO LA NDOA....ASEMA HAMPENDI, SIYO CHAGUO LAKE

  Malunde       Thursday, April 15, 2021
Mwanamke aitwaye Happy Nyasumo (18) mkazi wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara amemuua mumewe, Bebe Mbogo (26) kwa madai kuwa hampendi na hakuwa chaguo lake zikiwa zimepita siku 14 tangu walipofunga ndoa.

Tukio hilo limetokea Aprili 14, 2021 saa 4 usiku katika kitongoji cha Pengo kijiji cha Iseresere ambapo inadaiwa chanzo ni mgogoro wa ndoa ambapo Happy alirudi kwao kwa madai kuwa hamtaki mumewe lakini huko kwao wakamlazimisha arudi kwa mumewe kwa maelezo kuwa hawawezi kurudisha ng'ombe waliochukua wakati wakimuozesha.

Diwani wa Majimoto, Johannes Masirori ambaye ni mjomba wa marehemu amesema Mbogo na Happy walifunga ndoa Machi 31, 2021 na kudai kuwa mwanamke huyo amekiri kufanya mauaji hayo.

"Kabla ya mauaji anadai kuwa mumewe alimlazimisha kufanya tendo la ndoa na baada ya kumaliza mwanaume alilala na yeye alipobaini amesinzia akachukua panga na kumkata mara tatu shingoni”,amesema.

Amesema baada ya kufanya kitendo hicho akiwa hana hofu Happy alikwenda kwenye nyumba ya mkwewe na kuchukua chakula na kuanza kula na kuwaonyesha panga alilokuwa ameficha na wakati watu wakilia na kusikitika kutokana na tukio hilo, Happy hakuwa na wasiwasi na aliwataka wasiojua wamtazame vizuri.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post