MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA AMSWEKA NDANI MKANDARASI ERASTO KWILASA NA MKEWE | MALUNDE 1 BLOG

Friday, June 19, 2020

MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA AMSWEKA NDANI MKANDARASI ERASTO KWILASA NA MKEWE

  Malunde       Friday, June 19, 2020
Bw. Erasto Kwilasa
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amemsweka rumande Mkandarasi anayejenga barabara mbalimbali katika Manispaa ya Shinyanga, Erasto Kwilasa  pamoja na mke wake kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kutomaliza kazi ya ujenzi wa barabara kwa wakati. 

Inaelezwa kuwa Mkandarasi huyo ameshindwa kumaliza kazi ya ujenzi wa barabara mbalimbali zikiwemo za Ugweto na Kitangiri katika manispaa ya Shinyanga. 

Mwandishi wetu wa habari amezungumza na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ambaye amekiri kumuweka ndani Mkandarasi huyo. 

“Siku ya Jumanne nilikagua barabara za Manispaa ya Shinyanga,Jumatano nikakagua barabara za Shinyanga vijijini. Tuliyokubaliana Jumanne kuwa hadi kufikia leo Ijumaa yawe yametekelezeka yeye hajatekeleza,hajafanya ndiyo maana leo nimeamua kumuweka ndani”,amesema Mboneko. 

“Barabara zote anazotengeneza hajamaliza ndiyo maana nimemuweka ndani yeye na mke wake ambaye naye ni Mkandarasi. Kule Kitangiri anatengeneza barabara hamalizi huko Ugweto kunakolalamikiwa nako hamalizi kujenga barabara”,amesema Mboneko.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post