WAHAMIAJI HARAMU 236 WAKAMATWA TANGA

Wahamiaji haramu 236 wamekamatwa mkoani Tanga kwa kuingia nchini bila kibali katika maeneo mbalimbali kwa kipindi cha Januari hadi Mei 16 mwaka huu.


Kaimu Ofisa Uhamiaji, Mkoa wa Tanga Salum Farahani amesema hayo leo Mei 16, wakati akizungumza na Mtanzania Digital na kuongeza kuwa wahamiaji hao wamekuwa wakiingia mkoani hapa kama njia kuelekea nchini Afrika Kusini.


“Wahamiaji hao walikamatwa kwa kipindi hicho kwa miezi tofauti tofauti ambapo 49 walikamatwa Januari, 77 walikamatwa Februari, 18 walikamatwa Machi, 26 mwezi Aprili huku 66 wakikamatwa kuanzia Mei mwaka huu.


“Idadi kubwa ya wahamiaji wanatoka nchini Ethiopia na ndiyo kundi kubwa linaloongoza kwa kukamatwa ambapo kwa kipindi hicho walikamatwa 140, wakifuatiwa ambapo wamekuwa wakifika nchini kwa kusafirishwa na Watanzania ambao nao waliokamatwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527