Tanzia : MWANDISHI WA HABARI STEPHEN KIDOYAYI AFARIKI DUNIA


Stephen Kidoyayi enzi za uhai wake
Uongozi wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) unasikitika kutangaza kifo cha mwandishi wa habari Stephen Kidoyayi kilichotokea leo Jumatano Mei 16,2018.

Stephen Kidoyayi ambaye alikuwa anaandikia gazeti la Jamboleo kabla ya kuhamia gazeti la Tanzanite na pia alikuwa mwalimu wa Buhangija Sekondari amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga alipofikishwa leo baada ya kuugua.

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu,amesema baba yake takribani siku nne alikuwa anaumwa na leo asubuhi alifikishwa hospitali akisumbuliwa na kifua/kukohoa na ilipofika saa saba mchana akafariki dunia.

Mwili wa marehemu utaagwa na kusafirishwa kutoka nyumbani kwake Buhangija Shinyanga Mjini Ijumaa Mei 18,2018 saa mbili asubuhi kwenda kijiji Itubukilo wilayani Bariadi mkoani Simiyu kwa ajili ya mazishi.

Stephen Kidoyayi ni miongoni mwa waandishi wa waandishi wa habari waanzilishi wa Shinyanga Press Club,na amewahi kuwa katibu mtendaji wa Shinyanga Press club na mpaka umauti unamfika alikuwa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Shinyanga Press club.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Stephen Kidoyayi.Amina.

Imetolewa na Kadama Malunde -Mwenyekiti SPC
Theme images by rion819. Powered by Blogger.