Wednesday, May 16, 2018

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIYEIBA MAHINDI YAKANASA KICHWANI

  Malunde       Wednesday, May 16, 2018
Mahakama ya Mwanzo Mlandizi mkoani Pwani imemuachia huru, kijana Frank Joseph (23) aliyeiba kiroba cha Mahindi debe 1 na kumnasia kichwani baada ya mlalamikaji kutofika mahakamani hapo mara 3 mfululizo.


Frank ambaye ni mkazi wa Mbezi Dar es salaam, ameachiwa huru na Hakimu Mfawidhi, Nabwike Mbaba wakati shauri hilo lilipoitishwa kwa ajili mlalamikaji (mtendewa) kutoa maelezo ya jinsi alivyoibiwa.

Hakimu Mbaba amesema kuwa kutokana na mlalamikaji (mtendewa) kushindwa kufika mahakamani hapo mara 3 mfululizo kutoa maelezo ya kuibiwa kwake anaifuta kesi huyo.

“Mtendewa ameshindwa kufika mahakamani licha ya kupewa wito mara 3 mfululizo, hivyo naifutilia mbali kesi hii na mshtakiwa kuanzia sasa upo huru,” amesema Hakimu Mbaba.

Awali mshtakiwa alishindwa kufikishwa mahakamani mara 2 mfululizo kutokana na gari la Magereza kuharibika.

Katika kesi hiyo namba 124/2018 Frank anadaiwa kutenda kosa la wizi May 3, 2018 saa 7 usiku maeneo ya Mlandizi ambapo aliiba Mahindi debe 1 likiwa na thamani ya Sh.20, 000 ikiwa mali ya Seve Seleman.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post