Thursday, April 12, 2018

WAZIRI : TFF HAIPO JUU YA SHERIA

  Malunde       Thursday, April 12, 2018
Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza imesema Shirikisho la soka nchini TFF limesajiliwa chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano hivyo shughuli zake zote zipo chini ya serikali.Mh. Shonza ameyasema hayo jana wakati akjibu swali la mbunge wa Singida Mjini Mussa Ramashani Sima ambaye alihoji kuhusu mamlaka ya Waziri katika kusimamia kazi za TFF ikiwemo mapato na matumizi ya shirikisho hilo kutokana na katiba ya TFF kutoruhusu kuingiliwa na serikali.


''TFF pamoja na viongozi wake wote, wanapaswa wanalazimika na hivyo wanatambua mamlaka ya Waziri, kwasababu katiba ya TFF inatambua kuwa TFF ni chombo cha mpira ambacho kimesajiliwa chini ya sheria ya Baraza la Michezo ya 1967 na marekebisho yake ya mwaka 1971'', alisema Shonza.


Aidha Mbunge Mussa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Singida amemuomba Waziri kuhakikisha wanaibana TFF ili ipeleka mpango kazi kwenye vyama vya mikoa ili kujua matumizi ya pesa za ruzuku zinazotolewa kwa shirikisho hilo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post