WAZIRI MWAKYEMBE ATAKIWA KUWACHUKULIA HATUA NANDY, BILL NAS KWA VIDEO YA UCHI MTANDAONI

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na mshauri wa masuala mbalimbali ya mahusiano Dr. Chris Mauki amefunguka na kutoa maoni yake kuhusu sakata la wasanii Nandy pamoja na Bill Nas kufuatia kuvuja kwa video yao wakiwa faragha.

Mauki ameitaka Wizara inayohusika na masuala ya sanaa ichukue hatua dhidi ya wasanii hao ili kudumisha maadili na nidhamu katika jamii hususani kwa wasanii ambao ni kioo cha jamii na kusewa endapo watafanya hivyo basi litakuwa funzo kwa wasanii wengine na watu wengine katika jamii. 

"Mheshimiwa waziri Mwakyembe, Naibu Waziri pamoja na baraza la sanaa chini ya ndugu Mwingereza. Tutaiona nia yenu ya dhati kabisa kwenye kudumisha maadili na nidhamu katika jamii na hususani kwa wasanii ambao wanajiita "kioo cha jamii" pale ambapo hamtoinyamazia hii hali ya kuanikwa mitandaoni matukio ambayo kiuhalisia yalihitaji privacy, ninasimama sehemu ya ndugu zao hao wahusika, sehemu ya wazazi wao, sehemu ya wadogo zao, na wengine wengi ambao waliwaona kama role models wao. Kulikoni majukwaani tuwaone kama vioo vya jamii na huku nyuma mitandaoni mnaiharibu kabisa ile picha mliyoichora machoni pa watanzania" 

Aidha Mauki aliendelea kusisitiza kuwa "Kama ilivyoenea katika public basi tujulishwe katika public ni hatua gani za kinidhamu zinafuata na onyo kwa wengine wenye fikra finyu na chafu kama hawa wanaohalalisha tabia za kingono mitandaoni. Masikio ya wenye akili na hekima yanasubiri kusikia kutoka kwenu viongozi wetu wenye mpini" alisisitiza Chris Mauki

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527