Wednesday, April 18, 2018

WAZAZI WATAKIWA KUWANUNULIA WATOTO WAO SARE ZA SHULE

  Malunde       Wednesday, April 18, 2018
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Charles Kabeho amewaomba wazazi kuwanunulia watoto wao sare za shule kwa kuwa serikali kwa sasa imewaondolea jukumu la michango na kazi kubwa ya wazazi ni kuwahudumia watoto.

Wito huo aliutoa jana wakati Mwenge huo ulipowasili mkoani Kigoma ambapo alisema anasikitishwa anapoona wanafunzi hawana sare na wengine wanavaa nguo ambazo hazifai kwenda nazo shule kwani ni kuwatesa watoto na kuwafanya wajione tofauti na watoto wengine katika jamii.

Alisema serikali imejitahidi sana kuhakikisha kila mtoto ana kwenda shuleni  na kuwaondolea mzigo huo wazazi na uchangiaji ambao seeikali unahitaji kwa wazazi ni kununua sare za shule na kujitolea kuanzisha ujenzi wa madarasa mzazi anapo shidwa kununua sare za shule ni kumnyima uhuru na haki mtoto na ni jukumu lake kumuhudumi mtoto.

"Nikiongelea sare za shule ninamaanisha nguo, shati na viatu vifanane na watoto wote wilayani nimeumia sana kuona kunabaadhi ya watoto wanavaa nguo na viatu ambavyo havipendezi, inapendeza kila mtoto awe na sare na kupata elimu bora", alisema Kabeho.

Aidha alisema kwa walimu hawaruhusiwi kumfukuza mwanafunzi wala kukusanya mchango wowote kwakuwa serikali imekataa michango hiyo na wanafunzi waendelee kupata elimu bila kusumbuliwa.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kibondo Louis Bura alisema kwa sasa Wazazi wamekuwa na muitikio mkubwa wa kuchangia wa kujitokeza kujenga vyumba vya madarasa na mpaka sasa wanafunzi wanaendelea kupata eimu bora na kwa mkoa wa Kigoma wilaya hiyo imeongoza katika matokeo ya kidato cha sita na cha nne.

Alisema wataendelea kusimamia elimu na kuendelea kuwashawishi wazazi kuwaleta watoto shuleni ili waweze kupata elimu bora kwa kuwa serikali inataka kila mtoto apate elimu.

Na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Charles Kabeho akizungumza- Picha zote na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post