Tuesday, April 10, 2018

WATOTO WAWILI WAFARIKI KWA KUDONDOKEWA UKUTA MVUA IKINYESHA MWANZA

  Malunde       Tuesday, April 10, 2018
Wakati mvua zikiwa zinaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi na kusababisha mafuriko, Jijini Mwanza watoto wawili wa familia moja wamefariki baada ya kudondokewa na ukuta kipindi mvua hizo zikinyesha zilizokuwa na upepo mkali.


Akizungumza kutoka kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Ahmed Msangi amesema watoto hao wamefariki majira ya usiku wa April 9 wakati wakiwa wamelala katika nyumba waliyokuwa wanaishi katika mtaa wa Buguku kata ya Buhongwa wilayani Nyamagana Jijini Mwanza.


Kamanda Msangi amewataja watoto hao kuwa ni Mariam Saimon (4) pamoja na Musa Baraka (2) huku majeruhi wakiwa watatu katika tukio hilo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post