Wednesday, April 4, 2018

Video & Picha : RC SHINYANGA ASHINDWA KUJIZUIA..ACHEZA LIVE NGOMA YA BHUDAGALA KWENYE UPANDAJI MITI KISHAPU ..SHUHUDIA HAPA

  Malunde       Wednesday, April 4, 2018
Maadhimisho ya wiki ya Upandaji miti kitaifa yamezinduliwa Jumanne Aprili 3,2018 katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga yakiwa na kauli mbiu ya 'Tanzania ya kijani inawezekana,Panda miti kwa maendeleo ya viwanda'.

Pamoja na zoezi hilo kuambatana na upandaji miti katika kijiji cha Mwatuju wilayani humo, pia Msanii maarufu wa nyimbo za asili Bhudagala Mwanamalonja kutoka Serengeti mkoani Mara alipata nafasi ya kutoa burudani kwa wakazi wa Mhunze akihamasisha wananchi kupanda miti kupitia wimbo maalumu alioupa jina la Tanzania ya kijani inawezekana.

Wimbo huo ulimvutia Mkuu wa mkoa wa Shinyanga ,Mheshimiwa Zainab Telack na kuamua kuingia uwanjani kucheza akiwa na mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha na video shuhudia mwenyewe hapa chini

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ZAINAB TELACK AKICHEZA NGOMA YA BHUDAGALA

BHUDAGALA AKIIMBA WIMBO MAALUM WA UPANDAJI MITI

SIKILIZA WIMBO WOTE HAPA CHINI


Msanii maarufu wa nyimbo za asili Bhudagala Mwanamalonja kutoka Serengeti mkoani Mara akiimba wimbo wa Tanzania ya kijani inawezekana katika uwanja wa SHIRECU uliopo katika mji wa Mhunze wilayani Kishapu.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga ,Mheshimiwa Zainab Telack (kulia) akicheza wimbo maalumu kuhusu upandaji miti ulioimbwa na Bhudagala (katikati) .Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga ,Mheshimiwa Zainab Telack akicheza ngoma ya Bhudagala
Bhudagala akiwa amenyoosha kidole wakati akiimba wimbo wa Tanzania ya kijani inawezekana
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanry akinyoosha kidole kuwaonesha kitu (Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (katikati) na mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba).
Wanenguaji wa Bhudagala Mwanamalonja wakicheza wimbo wa Tanzania ya kijani inawezekana
Wanenguaji wakifanya yao
Ngoma imekolea....
Bhudagala Mwanamalonja akicheza na wanenguaji wake
Burudani inaendelea..
Mambo ni motoooo!!
Wanenguaji wakiendelea kuonesha vitu...
Mbwembwe sasa......
Burudani inaendelea...
Msanii maarufu wa nyimbo za asili Bhudagala Mwanamalonja huambatana na vijana wa sarakasi...wanaendelea kutoa burudani....yaani kila kitu balaaaa!!

Vijana wa Bhudagala wakiendelea kufanya mambo...

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Soma pia>>Picha & Video : MSANII MAARUFU WA NYIMBO ZA ASILI BHUDAGALA AKITAMBULISHA NYIMBO ZAKE MPYA 2018 LEO KISHAPU - SHINYANGA...NI BALAA!!
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post