Saturday, April 7, 2018

RAIS MAGUFULI: SITAKI JESHI LA POLISI LITUMIKE KUFYEKA BANGI ....KWA NINI MKAFYEKE BANGI?

  Malunde       Saturday, April 7, 2018
 Rais John Magufuli ameagiza askari kuwakamata wazee, wanawake, vijana na watoto wa maeneo yanapobainika mashamba ya bangi akieleza kuwa wakikamatwa watasema ukweli na watazifyeka wenyewe.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Aprili 7 wakati akizungumza na wakazi wa Arusha Uwanja wa Sheikh Amri Abeid baada ya kuzindua kituo cha polisi na nyumba 31 za polisi.

Rais Magufuli amesema kazi ya kufyeka mashamba ya bhangi ni ya wananchi wenyewe wanaolima bhangi hizo na kwamba askari hawakuajiriwa kwenda kufyeka mashamba ya bhangi.


“Sitaki Jeshi la Polisi litumike kufyeka bangi, kwa nini mkafyeke bangi? Tumieni intelijensia yenu mkakae pale kijijini na mtajua nani anakwenda kukagua mashamba hayo,mtaumwa nyoka mle, mna uniform nzuri msidhalilishe jeshi kwa kufyeka bhangi, nyie shikeni wote katika hicho kijiji, kamateni wote, wazee, wanawake hata watoto shika, ndipo watasema ukweli,” amesema.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post