Wednesday, April 18, 2018

POLEPOLE AWACHIMBA MKWARA WAPINZANI WANAOPONDA RIPOTI YA CAG

  Malunde       Wednesday, April 18, 2018
 
Chama cha Mapinduzi(CCM) kimesema kuwa kuna viongozi wa upinzani wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kuupotosha umma, tabia ambayo haikubaliki, haivumiliki na itafika wakati watasema sheria ichukue mkondo wake maana wanaleta taharuki kwa wananchi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole amesema hayo leo Jumatano Aprili 18 wakati akifafanua mambo kadhaa yanayopotoshwa katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).

Polepole amesema imekuwa tabia na mtaji wa kiongozi huyo ambaye hakumtaja jina kutoa taarifa za uongo.


“Kiongozi unasema fedha zimeibiwa sijui akiambiwa atoe ushahidi atasemaje. Siku hizi hana hoja ana kazi ya kuleta taharuki kwa umma,” amesema Polepole

“Hatuko tayari kuendelea kuona watu wachache wanauhadaa umma.”

Amesema CCM hakiamini malumbano, mabishano yasiyo na tija, lugha za kubeza, kebehi na kufifisha moyo wa kizalendo kwa Watanzania.


“Nchi yetu ina mfumo wa kidemokrasia ya vyama vingi lakini CCM inaendelea kuamini sisi ni wamoja.”


Na Elizabeth Edward, Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post