Tuesday, April 10, 2018

NYUMBA 12 ZASOMBWA NA MAJI DAR

  Malunde       Tuesday, April 10, 2018
Nyumba 12 zilizopo kando ya Mto Msimbazi,Mtaa Majengo Eneo la Vingunguti jijini Dar es salaam zimesombwa na maji na huku nyingine zaidi ya 100 ziko hatarini kuanguka kutokana na mmomonyoko wa udongo unatokana na kupanuka kwa Mto Msimbazi na kuingia katika makazi ya watu.


Baadhi ya wananchi wanaoishi katika mtaa huo wamesema hali ni mbaya katika eneo hilo, kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha huku mto huo ukiendelea kutanuka baada ya kuacha njia yake ya asili na kuingia katika makazi yao.


Diwani wa Eneo hilo Omar Kumbilamoto amesema walifanya juhudi za kupambana na mto huo kwa kuwashirikisha wananchi ambao kiasi cha Million 2 zilichangwa, lakini alidai baadhi ya watumishi katika manispaa hawakuonyesha ushirikiano na kuomba wizara ya mazingira chini ya ofisi ya makamu wa rais kuingilia kati.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post