Thursday, April 26, 2018

MZEE MAJUTO : NIKIFA MTAPATA TAARIFA

  Malunde       Thursday, April 26, 2018
Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Amri Athuman maarufu Mzee Majuto amefunguka na kuwatoa wasiwasi wapenzi na mashabiki wake kiujumla kuwa yeye ni mzima kabisa na endapo Mungu atamchukua 'kufariki' basi watapata habari popote pale watakapo kuwepo.

Mzee Majuto ametoa kauli hiyo baada ya siku za hivi karibuni kuzushiwa kifo kwa mara nyingine tena baada ya yeye kuzidiwa na kurudishwa hospitalini kwa mara nyingine ili aweze kupatiwa matibabu juu ya ugonjwa unaomsumbua.

"Mimi ni mzima kabisa, watu msiwe na wasiwasi kama nikifa mtapata habari nyote kwamba mimi tayari nimeshaaga dunia na sina wasiwasi kwa sababu wazazi wangu wote hawapo, mtume wangu ninayempenda Mohamed (S.A.W) naye pia hayupo sasa sembuse mimi msihofu sana jamani", amesema Mzee Majuto.

Siku ya Jumatatu Aprili 23, 2018 Mzee Majuto alilazwa katika Hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam, baada ya kuzidiwa. Awali Majuto alilazwa hospitalini hapo mnamo Januari mwaka 2018 na kufanyiwa upasuaji wa ugonjwa wa tezi dume ambao ndio umekuwa ugonjwa wake mkubwa unaomsumbua kila mara.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post