MBWA WAUA WATU WATANO MOSHI

 
Watu watano wamefariki dunia wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro baada ya kung’atwa na mbwa wenye kichaa.

Daktari bingwa wa magonjwa ya dharura na ajali wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Dk Francis Sakita amewaambia wanahabari leo Aprili 12,2018  kuwa ugonjwa huo umekuja kwa kasi kubwa ukilinganisha na miaka mingine.

Amesema kwa kipindi cha Januari hadi Machi vimetokea vifo vitano.

"Hii sio hali ya kawaida kutokea idadi kubwa ya watu kufariki dunia kwa kung'atwa na mbwa wenye ugonjwa huu, idadi hii ni kubwa sana na wengi walioathirika ni watu ambao wako Moshi vijijini. Hii inatokana na watu kutozingatia kupeleka mbwa wao kwenye chanjo," amesema Dk Sakita.
Na Janeth Joseph, Mwananchi
Theme images by rion819. Powered by Blogger.